Na Said Mwishehe, Michuzi TV


KAMISHINA wa Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya( DCEA) Dk.Peter Mfisi amesema suala la kuhalalisha kilimo cha bangi sio jambo jepesi kama baadhi ya watu wanavyofikiria.

Ametoa kauli hiyo leo Novemba 13, 2023 alipokuwa akijibu baadhi ya maswali ya Wahariri wa vyombo vya habari nchini wakati wa semina iliyoandaliwa na Mamlaka hiyo kwa wahariri hao.

Akijibu swali la kwanini Serikali isiruhusu kilimo cha bangi ili kuuza nje ya nchi ili kupata kipato, Dk.Mfisi amesema sio jambo rahisi kuhalalisha kilimo hicho huku akieleza kuwa nchi ambazo zimeruhusu kilimo cha bangi wameweka na utaratibu ukiwemo wa bangi kulimwa katika Green House ili kukidhi ubora unaohitajika katika soko.

"Bangi yetu inalimwa katika maeneo ambayo hayako katika utaratibu hivyo hata kuuza katika sokoni haiwezekani lakini nchi ambazo zinaruhusu kilimo hicho wameweka vigezo vinavyotakiwa.Lakini nchi ambazo zimeruhusu kilimo cha bangi au kutumia bangi wameweka na umri ili kuepusha watoto kuvuta.

" Mtoto mdogo ubongo wake unaendelea kukua, hivyo akivuta bangi kunamsababisha athari, ndio maana mtoto hawezi kuruhusiwa kutumia, "amesema na kufafanua bangi inatumika katika kutengeneza dawa lakini ni bangi iliyolimwa kwa utaratibu unaotakiwa.

" Sio bangi zote zinatumika kutengeneza dawa, bali zipo bangi ambazo zimekidhi viwango vinavyotakiwa.Hata hivyo takwimu zimebainisha nchi zilizohusu kilimo cha bangi zimebainika kuongezeka kwa matukio ya uhalifu pamoja na afya ya akili."


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...