Na. Zainabu Ally - Saadani.

Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara, Herman Batiho amewataka Maafisa na Askari wa Jeshi la uhifadhi, Hifadhi ya Taifa Saadani kuzingatia maadili na uzalendo katika kutekeleza majukumu yao ili kujiepusha na viashiria vya rushwa na matumizi ya madawa ya kulevya.

Ameyabainisha hayo Oktoba mosi, 2023 alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Hifadhi ya Taifa Saadani.

Kamishna Batiho alisema, "licha ya kufanya kazi kwa kufuata misingi ya taaluma zenu, niwatake pia mfuate sheria na taratibu za Jeshi la Uhifadhi ambayo inawataka muwe na nidhamu, uzalendo, uwajibikaji na ushirikiano baina yenu na vyombo vingine vya ulinzi na usalama".

Aidha, Kamishna Batiho aliwasisitiza maafisa na askari kuendelea kutunza vyema vitendea kazi vilivyotolewa na Serikali katika kuendeleza na kuboresha huduma za Uhifadhi na utalii katika hifadhi hiyo yakiwemo magari na mitambo inayotumika katika ukarabati wa miundombinu.

Kamishna Batiho pia, aliwasisitiza watumishi kuishi katika kiapo chao katika kufanya kazi mahali popote na katika mazingira yeyote yale ambayo mtumishi atapangiwa.

Aidha, "kwa kufanya kazi kwa bidii mtaongeza tija na kuifanya Hifadhi ya Taifa Saadani iendelee kuwa ni miongoni kwa Hifadhi za kimkakati, jambo la pili muitangaze sana kutokana na upekee wa vivutio vyake, italiongezea taifa mapato mengi zaidi tofauti na ilivyo sasa", aliongeza Kamishna huyo.

Hifadhi ya Taifa Saadani ni hifadhi pekee nchini Tanzania ambayo nyika na Bahari ya Hindi hukutana na kuifanya iwe na vionjo tofauti unapoitambelea.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...