Na Mwandishi Wetu

CHAMA Cha Mapindizi (CCM), kimeridhishwa na uongozi wa Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi.

Hayo yamesemwa leo Novemba 4, 2023, na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana, katika maadhimisho ya miaka mitatu ya uongozi wa Dk. Mwinyi.

Kinana amesema Dk. Mwinyi amejituma sana na kujikita katika kuleta maendeleo ya wananchi wa Unguja na Pemba huku akiwaunganisha kuwa kitu kimoja.

Akiyataja mafanikio yaliyopatikana Zanzibar kwa miaka mitatu tangu Rais Dk. Mwinyi alipoingia madarakani, Ndugu Kinana amesema ni pamoja na kuharakisha maendeleo kwa kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa shule, hospitali na miradi ya wananchi ya kiuchumi.

Aidha, amesema amewaunganisha wananchi, hivyo kusahau tofauti za itikadi za kisiasa, na watu wote kuwa wamoja.

Ndugu Kinana amefafanua kwamba, hatua hiyo inatoa matumaini katika kipindi cha miaka miwili iliyobakia kufikia ukamilikaji wa malengo ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.

"Rais Mwinyi tunakushuru sana, katika kipindi cha miaka mitatu umefanya mambo makubwa, ikiwemo kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi, pamoja na kuwaunganisha wananchi na kuimarisha amani na utulivu wa kisiasa," amesema Ndugu Kinana.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...