Na.Khadija Seif Michuziblog

KAMPUNI ya "The Look Company" imezindua rasmi kauli mbiu itakayotumika katika Mashindano ya Urembo Miss Tanzania kwa mwaka 2024 (Urembo na uongozi) huku akiwataka Mawakala wa mashindano hayo kulenga zaidi kuwaanda warembo kuwa viongozi bora kusaidia taifa la Tanzania katika nyanja mbalimbali.

Akizungumzana Wanahabari pamoja na Mawakala wa Shindano la Miss Tanzania kwa upande wa Mikoani na Kanda za Vyuo vikuu Afisa Sanaa Mwandamizi kutoka Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Agustino Makame amewapongeza Kampuni ya "The Look" kwa kuendesha mashindano hayo ya urembo kwa takribani miaka mitano na kubadilisha maisha ya wasichana wengi.

Aidha ,Makame ameeleza kuwa mashindano hayo ni sehemu ya kuibeba Sura ya nchi kwani Mrembo anaechaguliwa katika ngazi ya Miss Tanzania anakwenda kuitangaza Tanzania katika Mashindano ya kidunia (Miss world) hivyo warembo hao wanatakiwa kujua wameibeba dhamana kubwa ya Taifa hilo.

Pis ametoa wito kwa wasanii na watu wote wanaojihusisha na kazi za sanaa kuhakikisha wanatambulika kisheria kwa maana ya kujisajiri baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kupata vibali vya kuendesha shughuli hizo za sanaa.

Nae Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Basilla Mwanukuzi amesema Mashindano hayo ya Urembo yamekuwa na ushawishi mkubwa na kumtengeneza mrembo kuwa Kiongozi na mtu maarufu na msaada kwa jamii yake tofauti na dhana iliyojengeka miaka ya nyuma kuwa urembo ni uhuni.

Mbali na hilo basi amefungua rasmi semina kwa Wakala wa shindano hilo ambao wamehudhuria akiwemo wakala kutoka Mtwara Rajab Mchata,Mariam kutoka kanda ya pwani pamoja na Adam Kundiya wakala kutoka kanda ya vyuo vikuu huku akisisitiza zaidi kwa mawakala hao waende kuwaandaa warembo kuwa viongozi bora watakaolisaidia taifa la Tanzania katika sekta mbalimbali kama warembo wengine walivoiacha alama nzuri kwa jamii na taifa kwa ujumla.

''Semina itahusisha mawakala wetu ambao wanatupa warembo kuingia kuchuana katika mashindano haya hivyo semina itajikita zaidi katika kuboresha na tunamuandaa vipi mrembo huyo tunaetarajia awe Kiongozi wa baadae."

Pia amesema Mashindano ya Urembo Miss Tanzania 2024 yamebeba sura mpya za mawakala kutokana na uwepo kwa wapiga picha na washereheshaji mbalimbali hivyo wanategemea kuwa na ushirikiano mkubwa kwa watu wenye maono tofauti tofauti kuingia katika fani ya urembo.

 

Picha ya pamoja kati ya Afisa Sanaa Mwandamizi kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wa kwanza kushoto akifatiwa na Mwakilishi kutoka Wakala wa Misitu (TFS) pamoja na Mkurugenzi wa ''The Look Company " Basilla Mwanukuzi akifatiwa na Miss Tanzania 2023 Trace Nabukera pamoja na mdhamini wa shindano hilo Amina (Itallaboutcards) wakati wakizundua kauli mbiu ya shindano hilo "Urembo na Uongozi " mapema Leo Novemba 27,2023 Jijini Dar es Salaam
 

Mkurugenzi wa "The Look Company " Basilla Mwanukuzi katikati,Kushoto kwake  akiwa na Miss Tanzania 2023 Trace Nabukera pamoja na Mrembo Fatma Suleman akiambatana na Nelly Kazi Kazi  katika Hafla ya uzinduzi wa kauli mbiu ya Mashindano hayo 2024  "Urembo na Uongozi "

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...