Na Shamimu Nyaki
 

Katibu Mkuu wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Gerson Msigwa amewataka Watumishi wa Wizara hiyo waongeze ubunifu katika utekekezaji wa Majukumu yao ili Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo ziendelee kuwanufaisha wananchi.

Katibu Mkuu Gerson Msigwa, ametoa rai hiyo Novemba 10, 2023 Mtumba Jijini Dodoma alipokutana na kufanya kikao na watumishi wa wizara hiyo, ambapo amewataka wawe mstari wa mbele katika kubuni, kuanzisha na kusimamia matukio mbalimbali ya michezo yenye lengo la kuinua ari ya wananchi kupenda michezo.

Ametoa wito kwa watendaji na watumishi wa wizara hiyo waongeze ubunifu katika kuanzisha programu zenye lengo la kuibua miradi itakayoendana na wakati uliopo kwa lengo la kukabiliana na changamoto zinazoikabili Sekta hiyo.

"Leteni mawazo mapya kwa kuandika miradi, ikibidi shirikianeni na Sekta binafsi ili Wizara yetu iwe na vyanzo vya mapato nje ya Bajeti ili tuweze kutekeleza vyema kazi zetu, ikiwemo kutoa furaha kwa watanzania na kupunguza madhara ya kiafya yanayotokana na watu kutokufanya mazoezi" amesisitiza Bw. Msigwa.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...