Na Sabiha Khamis , Maelezo

Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Mahmoud Mohamed Mussa ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Jiji, amewataka Watendaji na Wananchi kuendelea kushirikiana ili kukabiliana na maafa yanayojitokeza katika kipindi cha mvua.

Akizungumza wakati wa kupokea taarifa ya utendaji kazi , huko Ofisini kwake Michenzani Mall, amesema kufanya hivyo kutasaidai kumarisha usafi wa Mji hasa katika Kipindi cha Mvua za Vuli zinzoendelea kunyesha.

Kufuatia chanagamoto zinazojitokeza katika kipindi cha mvua Mstahiki huyo aliwataka watendaji wa Baraza hilo kuendelea kusafisha mitaro na kuondoa majaa yasiyo rasmini ili kuzuia madhara yasiotokee kwa kasi zaidi.

“Endapo hatukufanya kazi ile ya kusafisha mitaro, kuondoa majaa yaiyokuwa sio rasmini basi maji yangelituathiri zaidi na hasara ingekuwa kubwa zaidi” alisema Mtahiki Meya.

Hata hivyo aliwapongeza madiwani, watendaji na taasisi zote zilizowajibika kuhakikisha kwamba inaisaidia Zanzibar hususani Mkoa wa Mjini Magharib kukabiliana na mvua zinazoendelea.

Awali Mstahiki Meya alitumia fursa hiyo kutoa pole kufuatia kifo cha kijana aliejitolea kusaidia kuzibua mtaro kwa maslahi ya Wananchi na wote walioathiriw a na mvua hizo kwa namna moja au nyengine

Hata hivyo alisema Baraza hilo litaendelea kuwajibika ipasavyo ili kuiarisha Mji kuwa safi na salama.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Baraza la Jiji Zanzibar Said Salmini Ufuzo akiwasilisha utekelezaji wa Baraza hilo alisema katika kipindi cha robo ya kwanza Julai hadi Septemba limefanikiwa kuanzisha programu ya kuwajengea uwezo madiwani na watendaji, kuwalipa stahiki Madiwani na watendaji wa ofisi, kutoa huduma za utendaji na utawala, kuzisimaia manispaa za jiji pamoja na kubuni na kuendeleza miradi ya maendeleo ya Baraza hilo.

Alielezea kuwa jumla ya watendaji thelethini wakiwemo madiwani, watendaji wa manispaa wa Mjini wamepatiwa mafunzo ya muda mfupi yanayohusiana na mfumo wa ukusanyaji taka ili kuboresha usafi wa Mji .

Nao baadhi ya wajumbe wa Baraza hilo wakiwasilisha utekelezaji wa kamati zao Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii na Mazingira Abdul-latif Omar Haji alisema katika kuhakikisha Mji wa Zanzibar unakuwa safi, jumla ya ndoo mia tano za kuhifadhia taka (dust bin) zimegaiwa katika maeneo mbali mbali ikiwemo vituo vya afya, maskulini, manispaa za jiji, madrasa pamoja na watendaji wa Baraza la jiji ili kuimarisha usafi nchini.

Pia kamati hiyo ilifanikiwa kukagua mitaro ya maji taka na majaa yasiyo rasmini ili kuweka mazingira bora kwa wananchi.

Kikao hicho kilijadili utekelezaji wa kazi za ofisis za baraza la jiji na kamati za kudumu za Baraza la jiji Zanzibar kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka iliyoanzia julai hadi septemba mwaka wa fedha 2023-2024.

Mstahiki Meya wa Jiji La Zanzibar Mahamed Mahmoud akizungumza katika kikao cha 12 cha Madiwani ambacho kilipokea  na Kujadili Taarifa za Utekelezaji wa Kazi za Ofisi ya Baraza la Jiji na Kamati za Kudumu za Baraza la Jiji la Zanzibar na Masuala mengine mbalimbali ,Kikao kilicho fanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Michenzani Mall.
Mwanasheria wa Baraza la Jiji la Zanzibar Zainabu Makame Sururu akifafanua na kujibu Baadhi ya maswali yalioulizwa katika  cha 12 cha Madiwani ambacho kilipokea  na Kujadili Taarifa za Utekelezaji wa Kazi za Ofisi ya Baraza la Jiji na Kamati za Kudumu za Baraza la Jiji la Zanzibar na Masuala mengine mbalimbali ,Kikao kilicho fanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Michenzani Mall.
Wajumbe wa Kikao cha 12 cha Madiwani wakisikiliza Dua ya Ufunguzi wa Kikao hicho Kilicho pokea na Kujadili Taarifa za Utekelezaji wa Kazi za Ofisi ya Baraza la Jiji na Kamati za Kudumu za Baraza la Jiji la Zanzibar na Masuala mengine mbalimbali ,Kikao kilicho fanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Michenzani Mall.
 

Mjumbe wa Kikao cha Madiwani Muheshimiwa Janeth Sekuhola akiwasilisha Taarifa katika kikao cha 12 cha Madiwani ambacho kilipokea  na Kujadili Taarifa za Utekelezaji wa Kazi za Ofisi ya Baraza la Jiji na Kamati za Kudumu za Baraza la Jiji la Zanzibar na Masuala mengine mbalimbali ,Kikao kilicho fanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Michenzani Mall.
 

Mwenyekiti wa Huduma za Jamii na Mazingira Baraza la Jiji la Zanzibar Abdul-latif Omar Haji akisoma Taarifa katika kikao cha 12 cha Madiwani ambacho kilipokea  na Kujadili Taarifa za Utekelezaji wa Kazi za Ofisi ya Baraza la Jiji na Kamati za Kudumu za Baraza la Jiji la Zanzibar na Masuala mengine mbalimbali ,Kikao kilicho fanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Michenzani Mall.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...