Na.Khadija Seif ,Michuziblog
TAASISI ya uandaaji matukio ya Wajasiriamali wa Kazi za Mikono (AFROPRENUER) wamekumbusha Makampuni,taasisi na Wafanyabiashara kukumbuka kurudisha kidogo kwa jamii ili kuweza kunusuru maisha ya Watanzania wengi kuliko kusubiri Serikali kutatua changamoto hizo kwani kwa sasa wagonjwa wengi wanasumbuliwa na matatizo mbalimbali mahospitalini.
Akizungumza na Wanahabari Leo Novemba 19,2023 Mkurugenzi wa Kampuni ya Uandaaji matukio ya Wajasiriamali wa kazi za Mikono ( AFROPRENEUR) Shadia Masoud amesema Kampuni hiyo inatarajia kufanya Maonesho ( DAR CHRISTMAS FAIR 2023) kuanzia disemba 08 hadi disemba 10 ,2023 kwa lengo la kuwakutanisha pamoja watoa huduma mbalimbali wa bidhaa za mapambano, nguo na vyakula kipindi hiki cha Sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya.
"Ni msimu wa tatu wa Maonesho ya Dar. Hivyo kama kawaida yetu tutakuwepo eneo la Seacliff Masaki na tunategemea kuwepo kwa Wauzaji wa Bidhaa za mapambano, nguo pamoja na Michezo ya watoto kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya."
Aidha Masoud ameongeza kuwa Taasisi hiyo imejijengea desturi ya Kurudisha kidogo kwa jamii inayowazunguka ambapo Mwaka jana waliweza kusaidia watoto 10 viti vya kusukuma ( Wheelchairs) katika hospitali Jijini Dar es Salaam hivyo kwa mwaka huu wanategemea kusaidia mahitaji mbalimbali watoto wenye vichwa vikubwa katika hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Mratibu wa Maonesho hayo Nasma Aboubakary amewaalika wadau mbalimbali kuhudhuria Maenesho hayo huku akisisitiza zaidi kuwa hakuna kiingilio badala yake waje kujipatia bidhaa nzuri zenye ubora zilizotengenezwa na Wajasiriamali wa Kitanzania lengo ni kuonyesha uzalendo wa bidhaa za kitanzania zaidi.
Pia amesema Wanatarajia Maonesho hayo kufungwa na Mgeni rasmi ambae ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto kufungua Maonesho hayo kwa Wajasiriamali zaidi ya 10 ambao wataendesha biashara kwa siku tatu mfululizo.
Mbunifu wa Mavazi kutoka Kampuni ya ( Pick Me Up ) Riziwan Remtulla amewaasa Wafanyakazi na Wajasiriamali wadogo kwa wakubwa kushiriki Maonesho hayo na mengine ili kuongeza maarifa na ufanisi katika kufanya biashara zao na kukutana na wateja wao huku likiwemo swala la kujitangaza zaidi.
"Kwa mara ya kwanza nashiriki Maonesho haya huku shahuku yangu kubwa kuona watanzania na wageni wanakuwa wazalendo na vitu vyenye ubunifu wa hali ya juu hivyo kampuni yangu ya "Pick Me up " ipo tayari kutoa huduma ya nguo zenye michiro ya kitamaduni yenye kuhamasisha utalii zaidi hivyo niwasihi Wajasiriamali wengine waweze kufika katika viwanja vya Seacliff Masaki Jijini Dar es Salaam kununua bidhaa zetu. "
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...