Na Shamimu Nyaki
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Wizara anayoiongoza itaendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa Kituo Cha Michezo katika Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Malya mkoani Mwanza kama ilivyopanga.
Dkt. Ndumbaro amesema hayo Novemba 6, 2023 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Sumve, Mhe. Kasalali Mageni aliyehoji kwanini wizara inahamisha ujenzi wa Kituo cha Michezo Malya kutoka Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza kwenda Ilemela wakati imeshasaini Mkataba wa utekelezaji.
"Tutaendelea na ujenzi wa Kituo Cha Michezo Malya kama ambavyo tumepanga, hatujahamisha ujenzi huo kwenda sehemu nyingine, lakini pia tutaendelea na ujenzi wa Kituo cha Michezo katika Wilaya ya Ilemela na maeneo mengine kwa kuwa azma ya Serikali ni kuwa na vituo pamoja na akademia za michezo katika maeneo mbalimbali nchini" amesisitiza Mhe. Ndumbaro.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...