Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Kitengo cha Utafiti kutoka Kampuni ya Orbit Securities Fortius Rutabingwa Amesema kuwa kama kweli wadau kwenye sekta wanataka kufanikiwa nimuhimu wakajiunga kwenye soko la hisa na hati fungani.
Amesema kama kweli wanataka kushiriki kwenye eneo hilo basi nivema kuwa kwenye soko la hisa kwani madini sio biashara ya haraka haraka ni safari ndefu na inahitaji uvumilivu lakini mwisho wake inalipa.
Rutabingwa ameyasema hayo kwenye ofisni za Kampuni hiyo zilizopo kwenye jengo la Golden Jubilee jijini Dar es Salaam ambapo Amesema sekta ya madini imekuwa na changamoto nyingi hasa za kimitaji hivyo kama kweli wadau wanataka kufanikiwa nivema wakajiunga kwenye soko la hisa na Mitaji pamoja na hati fungani.
"Ufanyaji wa shughuli za madini unahitaji ghrama kubwa na Utafiti wa kina juu ya kubaini mahala unapokwenda kuchimba pana mali au laa hivyo ili ufanye hivyo pia panahitajika kuwa na watalaamu na ili uweze kuwa na nguvu hiyo inahitaji mitaji ya kutosha kama ilivyo Kwa makampuni makubwa ambayo Leo wanafanya vizuri, "amesema Rutabingwa
Akitolea mfano Kampuni kama GGM inazalisha Kwa kiasi kikubwa lakini kabla yake palikuwepo na Kampuni ya utafiti ambayo ilikaa kwenye eneo hilo kwa zaidi ya miaka 10 kabla ya kufikia hatua waliyonayo sasa ya uzalishaji.
Ameongeza hata Barick na kwenyewe kulikuwepo na kampuni za utafiti kabla ya kuaza kuzalisha kwahiyo watu wanapoingia kwenye sekta hiyo wajue hilo kinyume na hapo inakuwa bahati tu ambapo unaweza kuingia na ukafanikiwa .
Rutabingwa amefafanua unawekeza kutokana na taarifa ambazo unazipata lakini inahitaji uvumilivu na kukubali kuwatumia watalaamu na wao kama orbit Securities ambao wapo tayari kuwashika mkono wachimbaji.
Amesema na kwa takwimu walizonazo wanauzoefu na njia za kupita hivyo wao wanaweza kusaidia kukupatia watalaamu ambao ni watafiti wenye vyeti kamili wakikaa hapo na kufanya utaalamu wao watakuja na taarifa za uhakika wa kile kilichopo pale chini.
Pia Amesema Kwa wadau kwenye sekta ya madini njia nyingine ya wao kuweza kufanikisha kile ambacho wanafanya nikukubali kujiunga kwenye masoko ya hisa ,mitaji na hati fungani Kwani wanahitaji mitaji mikubwa ili kuweza kufanya shughuli za kwenye madini kinyume na Sasa ambapo wamekuwa wakilia kuhusu kukopeshwa fedha kupitia mabenki.
Akizungumzia madhumuni ya kuazishwa kwa Orbt Securities Fortius Rutabingwa amesema kuwa kazi kubwa ya Kampuni hiyo ni kutoa huduma ya ushauri wa masuala ya uwekezaji pamoja na kufanya biashara kwenye soko la Hisa .
Amesema kazi nyingine ni kushauri wajasiliamali au makampuni mengine ambayo yanataka kutafuta mitaji kupitia Soko la Hisa ambapo wao orbit Securities ni kampuni ambayo iliaza tu Soko lilipo aza.
Ameongeza Soko la Hisa lengo lake ni kufanya mageuzi ya kiuchumi na kifedha Tanzania na kwamba ilifikia mahala nakuona nivizuri kuwepo na makampuni ambayo yanaitwa makampuni ya umma hivyo mtu yeyote ana hisa za Akiba anaweza kuwekeza na akaweka Akiba yake binafsi na anaweza kushiriki kumiliki makampuni ambayo yanaendesha Hisa .
"Makampuni mengi ambayo yanaendesha Soko la Hisa mwanzoni yalikuwa ya Serikali ambapo Serikali wakaamua kuyabinafisisha kwa kuuza hisa zao kwa umma kwa watu binafsi na kwa mashiriki...
"Kwahiyo mtu yeyote ambaye ana akiba na anataka kuwekeza ikawa ni njia nzuri zaidi na Yeye kuwekeza ili kuweza kuingiza faida hivyo mtu ambaye amenunua hisa kwenye hiyo Kampuni na kumiliki katika kiwango ambacho amewekeza anatakiwa kupata faida kama hiyo Kampuni inatengeneza faida, "amesema Rutabingwa .
Amefafanua kwenye kupata faida ni kwamba unaweza kuweka Sh. 100,000 na inaweza kuongezeka hivyo unaweza kuamua kuuza na ukachukua faida na pia kwenye soko hilo kuna bidhaa nyingine ambapo Serikali huwa inakopa jwa umma kwa kutoa hati fungani ambapo zilitolewa huwa zinarudishwa kwenye soko la hisa kama mwekezaji ambaye amekuwa amenunua kwenye mnada wa awali anaweza kuuza kwenye soko la hisa mfano akinunua hati fungani miaka 25 sio lazima ukae naye miaka hiyo hivyo unaweza orodhesha kwenye soko la hisa na unaweza kuuza au vinginevyo.
"Mtanzania yeyote ambaye anaumri wa juu ya miaka 18 anaweza kuingia kwenye soko la hisa hakuna masharti magumu na unachotakiwa kuwa nacho kwenye soko la hisa uwe na kipanda uso ambapo utajaziwa fomu na kufungulikuwa akaunti hapo tayari utakuwa umeingia kwenye soko la hisa na baada ya hapo muda wowote unaweza kuwekeza labda kwenye soko hati fungani huko unahitajika uwe na picha Moja na kitambulisho pamoja Tin utafunguliwa akaunti na muda wowote unaweza kuwekeza.
Pia amesema kwenye hati fungani za Muda mfupi kiwango cha chini cha kuaza nacho ni sh.laki 500,000 na zile za Muda mrefu kiwango cha chini cha kuazia ni sh.1000,000 lakini kwenye soko la hisa kimsingi hakuna kiwango cha chini hata sh 10,000 au 50000 unaweza kuaza kuwekeza na kiwango cha chini kinawekwa endapo unaingia kwenye soko hilo Kwa mara ya kwaza .
KUHUSU SERIKALI
Rutabingwa amesema serikali wao ndio wanatoa leseni ya mambo yote wanayofanya mfano Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(SMSA) ndio unakuta leseni ya kushiriki kwenye soko la hisa.
Amefafanua kwahiyo wao kama orbit ndio wadau na wanapeleka taarifa mbalimbali ya kile kinachoendelea na inabidi wafanye kazi Kulingana na misingi waliyowekewa ikiwa pamoja na kufuata viwango ambavyo vimewekwa na Mamlaka ya masoko na mitaji.
Amesema hata upande wa Benki kuu wao ndio wanatoa kibari cha kushiriki kwenye mnada wa hati fungani hivyo na wao wanakagua ushiriki wao kwenye maeneo mbalimbali Kulingana na misingi ambayo imewekwa .
Kuhusu umuhimu wa kwenye soko
Rutabingwa Amesema kuwa umuhimu wake kwasababu watu wapo kwenye shughuli za kiuchumi lazima kuwepo na nidhamu ya pesa ambayo nivizuri ukawa unajiwekea akiba, hivyo kuweka akiba haitakiwi kuishia hapo.
Ameongeza lakini inatakiwa uanze kuwekeza kwani ukiweka Akiba bila kuwekeza unaweza kutumia bila kujua ndio maana lazima uwekeze hivyo ni njia nzuri ya Akiba Yako kuiweka
Ameongeza kuwa kwasababu faida utakayoipata kwenye soko la hisa au kwenye hati fungani mara nyingi inakuwa kwenye mfumko wa bei kwahiyo uwepo wa soko hilo inamsaidia kila mtu iwe kampuni au binafsi ,au mashirika ni jinsi ya kuwa na nidhamu ya fedha.
Pia amesema ili kuweza kuwasiliana nao basi wasiliana nao kwa kutembelea website mitandao ya kijamii Kwa jina orbit Securitie
Mkuu wa Kitengo cha Utafiti kutoka kampuni ya Orbit Securities akifanya mahojiano na Dmnewstz ofisini kwake jijini Dar es Salaam kuhusu umuhimu wa makampuni ,mashirika na wadau kwenye sekta ya madini kujiunga kwenye soko la hisa na mitaji pamoja na hati fungani ili kurahisisha shughulizao na kuweka Akiba ya baadae

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...