Katika kuhakikisha wanaendelea kusogeza huduma za kifedha karibu na wananchi, Shirika lisilo la kiserikali BRAC Tanzania Finance Limited limetanua wigo wake wa kihuduma kwa kuzindua matawi mawili mapya katika Mkoa wa Ruvuma.

Uzinduzi huo wa matawi ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya shirika hilo ya kufikisha huduma za fedha karibu kwa watu wanaoishi katika mazingira yasiyofikika kirahisi hususani wanawake.

Matawi hayo yamezinduliwa katika Wilaya ya Tunduru na Madaba na kwa Mwaka huu wamezindua jumla ya matawi mapya 13 ili kuendelea kupanua huduma zetu wakiwa na lengo ya kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika jamii zetu nchini.

BRAC Finance Tanzania inatoa huduma za kifedha kupitia mikopo midogo midogo kwa wajasiriamali na wakulima hasa wanawake na kwa sasa ina jumla ya matawi 177 yanayopatikana katika wilaya Zaidi ya 80 nchini kote.
Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba, Adv. Sajidu L. Mohamed (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la BRAC, tukio hilo lilishuhudiwa na Mh. Diwani wa Kata ya Lituta, Orasmo Pili (katikati), Meneja Mkuu wa BRAC Kanda ya Dodoma, Bi. Roda Hassan (Kushoto), Pamoja na wafanyakazi wa BRAC (nyuma) katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika ofisini hapo Madaba mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Sande Mtatiro akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi la BRAC Tanzaia Finance Ltd wilayani humo, mkoani Ruvuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...