Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Mha. Charles Sangweni amelipongeza baraza hilo kwa mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na Mamlaka kutokana na utendaji wa baraza hilo.
Mha. Sangweni ameyasema hayo kabla ya kulivunja rasmi baraza hilo la kwanza katika kikao chake cha saba, kutokana na baraza hilo kufikia ukomo wake kwa mujibu wa mkataba ulioingiwa baina ya PURA na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE).
“Tunajivunia kazi kubwa iliyofanywa na baraza hilo katika kuchochea maendeleo ya taasisi ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa ushirikishwaji wa watumishi katika maamuzi na utekelezwaji wa majukumu mbalimbali ya PURA,” alieleza.
Aliongeza kuwa kutokana na ushirikishwaji huo, wafanyakazi wamepata motisha zaidi ya kufanya kazi kwa ari, ushirikiano na ubunifu na hivyo kuiwezesha taasisi kuendelea kutimiza majukumu yake katika shughuli za mkondo wa juu wa petroli.
Mha. Sangweni alibainisha kuwa Baraza la Pili litaanza kazi rasmi mwezi Januari 2024 kwenye kikao chake cha kwanza ikiwa ni baada ya kufanyika uchaguzi wa wajumbe wapya kwa ngazi ya taasisi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania-TUCTA, Heri Mkunda amelipongeza baraza hilo kwa kazi waliyoifanya na kutoa pongezi mahususi kw menejimenti ya PURA kwa kuendelea kutengeneza mazingira bora ya kazi kwa wafanyakazi ili kuboresha utendaji wao.
Ametoa pia rai kwa wafanyakazi wa Mamlaka kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi mapana ya taifa kupitia sekta ndogo ya mafuta na gesi nchini.
“Mna wajibu mkubwa wa kufanya kazi kwa bidii, kwa kujituma na kushirikiana ili kutimiza malengo na majukumu yaliyokasimiwa kwa taasisi kwa mujibu wa sheria na miongozo ya nchi,” aliongeza.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa PURA wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kikao cha saba na cha mwisho cha baraza hilo la kwanza, kilichofanyika hivi karibuni.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa PURA wakiwa kwenye kikao cha saba na cha mwisho cha baraza hilo la kwanza, kilichofanyika hivi karibuni.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi PURA wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa kikao cha saba na cha mwisho cha Baraza hilo la Kwanza kilichofanyika hivi karibuni.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Mha. Charles Sangweni amelipongeza baraza hilo kwa mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na Mamlaka kutokana na utendaji wa baraza hilo.
Mha. Sangweni ameyasema hayo kabla ya kulivunja rasmi baraza hilo la kwanza katika kikao chake cha saba, kutokana na baraza hilo kufikia ukomo wake kwa mujibu wa mkataba ulioingiwa baina ya PURA na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE).
“Tunajivunia kazi kubwa iliyofanywa na baraza hilo katika kuchochea maendeleo ya taasisi ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa ushirikishwaji wa watumishi katika maamuzi na utekelezwaji wa majukumu mbalimbali ya PURA,” alieleza.
Aliongeza kuwa kutokana na ushirikishwaji huo, wafanyakazi wamepata motisha zaidi ya kufanya kazi kwa ari, ushirikiano na ubunifu na hivyo kuiwezesha taasisi kuendelea kutimiza majukumu yake katika shughuli za mkondo wa juu wa petroli.
Mha. Sangweni alibainisha kuwa Baraza la Pili litaanza kazi rasmi mwezi Januari 2024 kwenye kikao chake cha kwanza ikiwa ni baada ya kufanyika uchaguzi wa wajumbe wapya kwa ngazi ya taasisi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania-TUCTA, Heri Mkunda amelipongeza baraza hilo kwa kazi waliyoifanya na kutoa pongezi mahususi kw menejimenti ya PURA kwa kuendelea kutengeneza mazingira bora ya kazi kwa wafanyakazi ili kuboresha utendaji wao.
Ametoa pia rai kwa wafanyakazi wa Mamlaka kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi mapana ya taifa kupitia sekta ndogo ya mafuta na gesi nchini.
“Mna wajibu mkubwa wa kufanya kazi kwa bidii, kwa kujituma na kushirikiana ili kutimiza malengo na majukumu yaliyokasimiwa kwa taasisi kwa mujibu wa sheria na miongozo ya nchi,” aliongeza.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi PURA wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa kikao cha saba na cha mwisho cha Baraza hilo la Kwanza kilichofanyika hivi karibuni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...