Wachimbaji
wadogo wa eneo la uchimbaji wa madini la Sekenke,Wilaya ya Iramba
Mkoani Singida leo wamepatiwa Leseni za uchimbaji na uchenjuaji wa
Madini.
Zoezi la kukabidhi Leseni hizo limefanya na Waziri wa
Madini Mh. Anthony Mavunde leo katika eneo la Sekenke kufuatia maombi ya
Mbunge wa Iramba Magharibi na Waziri wa Fedha Mh. Dkt Mwigulu Lameck
Nchemba aliyoyawasilisha kwa Mh Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wakati wa
ziara yake ya kikazi mkoani Singida.
Akitoa maelezo ya
awali,Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Yahaya Samamba amesema
eneo ambalo linatolewa leseni ni eneo ambalo lilikuwa na Leseni ya
utafiti ambayo imeisha muda wake wa uhuishaji na kurejea serikali kwa
mujibu wa Sheria.Jumla ya Maombi 88 ya Leseni yamepokelewa na kufanyiwa
kazi katika eneo hilo ambapo ni maombi 28 tu ndio yamekidhi vigezo.
Akihutubia
umma wa wachimbaji,Waziri Mavunde amesema ni maelekezo ya Mh Rais Dkt.
Samia Suluhu Hassan kuwapatia maeneo ya uchimbaji wachimbaji wadogo kwa
lengo la kuongeza ushiriki wao katika sekta ya Madini na hivyo kuchochea
ukuaji wa uchumi.
Waziri Mavunde amewataka wachimbaji waliopewa
leseni kuzitumia kwa kufanya shughuli za uchimbaji kwa kuzingatia sheria
na kanuni bora bila kusahau kulipa kodi na tozo ili kuongeza mchango wa
sekta ya madini katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Mh. Peter J. Serukamba amesema uamuzi wa kuwapa Leseni
wachimbaji hao kupitia maelekezo aliyotoa Mh Rais Dkt Samia S. Hassan
yatachochea ukuaji wa uchumi wa wananchi wa Iramba na serikali itaongeza
mapato yake yatokanayo na kodi na ushuru mbalimbali na hivyo kuongeza
mchango wa mkoa wa Singida kwenye mapato ya serikali yatokanayo na
maduhuli ambapo kwa mwaka huu wa fedha Singida imepewa lengo la
kukusanya Bilioni 12 kwa mwaka na mpaka sasa wameshakusanya Bilioni 6
kabla ya robo ya pili.
Naye Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi
na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba kwa niaba ya wachimbaji wa
Sekenke amemshukuru sana Mh Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kufuatia
maombi ya wachimbaji hao kupatiwa leseni na kuahidi kwamba watahakikisha
maeneo hayo ya uchimbaji yanakuza uchumi wa wachimbaji hao na Taifa kwa
ujumla huku akiwaahidi kuwaunganisha na Taasisi za fedha kwa ajili ya
kupata mikopo na mitaji ya kuendesha shughuli zao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...