KESI ya shambulio la mwili inayomkabili mfanyakazi wa benki , Ibrahim Masahi ambae anatuhumiwa kumshambulia kwa nyundo jirani yake Deogratus Minja inatarajia kuendelea kusikiliza Desemba 7, mwaka 2023 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam.

Masahi anatuhumia kumshambulia kwa nyundo jirani yake huyo, baada ya Minja kwenda kumshitaki Serikali za Mitaa kwamba anatililisha maji mchafu katika eneo lake.

Mahakama hiyo, ilipanga tarehe mwishoni mwa wiki na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Amos Rweikiza, baada ya upande wa mashitaka kutokuwa na shahidi wa kuendelea kutoa ushahidi, kutokana na shahidi aliyetakiwa kupata udhuru.

Wakili wa Serikali, Salma Jafari amedai kuwa shahidi ambae alipangiwa kutoa ushahidi wake ni askari, ameshindwa kufika mahakamani kwa sababu anasimamia mitihani ya kidato cha nne inayoendelea nchi nzima.

Amedai kuwa kwenye orodha yake shahidi aliyetakiwa kuwepo kwa ajili ya kuendelea kutoa ushahidi ni askari polisi mpelelezi, ambapo hakufika mahakamani kwa sababu anaesimamia mitihani ya kidato cha nne.

Baada ya wakili kudai hayo, Hakimu Rweikiza aliwaeleza upande wa mashitaka kwamba kesi hiyo inatakiwa kuendelea kusikilizwa kwa sababu inatakiwa kuisha mwezi watatu.

" Mshitakiwa dhamana yako inaendelea hadi Desemba 7,2023, upande wa mashitaka walete shahidi kesi iendelee kusikilizwa," amesema Hakimu Rweikiza.

Masahi anatuhumiwa Januari 11, 2023 akiwa eneo la Mbezi Msakuzi ndani ya Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam alimpiga Deogratus Minja kwa nyundo na kumsababishia kupata madhara makubwa ya mwili mwake.

Katika ushahidi wake, Minja amedai kuwa tarehe hiyo saa mbili na nusu usiku alikuwa akipita nje ya geti la jirani yake Masahi, alimkuta kijana wa jirani huyo, baada ya kumuona alizungumza kwa kilugha kwa sauti kubwa ambae yeye hakuielewa.

"Ghafla kijana alikuja mbele yangu akanizuia nisipite, mara geti likafunguliwa akatoka Masahi akanihoji kwamba mimi ni kama nani na kwenda kumshitaki Serikali za Mitaa, sikumjibu chochote kijana wake akanipiga ngumi," amedai Minja

Minja aliendelea kudai kuwa, alimgeukia jirani yake ili amkataze kijana wake, lakini na yeye aliinua shati lake akatoa nyundo akampiga nayo kichwani, baada ya kupata maumivu makali alianza kukimbia huku akipiga kelele za kuomba msaada.

Amedai kuwa, alianguka chini ndipo Masahi akaanza kumshambulia tena na nyundo mgongoni, maumivu yalipomzidi aligeuka, akampiga na nyundo kwenye mkono wa kulia na kwenye bega.

"Jirani yangu Fadhili alifungua geti lake ndipo na mimi nikakimbilia kwake, alianza kunsaidia kwa sababu nilikuwa navuja damu nyingi alinilaza chini akafanya utaratibu akanipeleka Hospitali ya Bochi kwa matibabu," Amedai Minja katika ushahidi wake.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...