Na Fauzia Mussa, Maelezo

Msajili wa Hazina wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Waheed Sanya amesaini na kuzindua kitabu cha muongozo wa usimamizi wa mali za umma kwa lengo la kudhibiti upotevu na uharibifu wa mali hizo.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Ofisini kwake Maisara Mjini Unguja amesema hatua hiyo itasaidia kutunza mali zinazonunuliwa na Serikali kwa gharama kubwa pamoja na kuwepo kwa matumizi mazuri ya fedha kwenye ununuzi wa mali hizo.

Alisema kitabu hicho kitasaidia kuweka utaratibu mzuri wa utunzaji wa mali za Serikali kuanzia kunuliwa kwake hadi kumalizika kwa muda wake wa matumizi.

Msajili huyo alifahamisha kuwa ofisi ya hazina itauweka muongozo huo katika mitandao ya kijamii ili kutoa fursa kwa kila mmoja kuweza kukisoma kitabu hicho na kukifanyia kazi.

Aidha alitumia fursa hiyo kuwaomba watendaji wa Serikali na jamii kwa ujumla kufuatilia na kukisoma kitabu hicho ili kufikiwa malengo yaliyokusudiwa.

Ofisi ya Msajili wa Hazina ilianzishwa kwa sheria namba 6 ya mwaka 2021 kwa lengo la kusimamia na kuhifadhi mali zote za umma kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mkuu wa mali Zanzibar Ramia Mohammed Ramia akizungumza katika hafla ya utiaji saini na uzinduzi wa kitabu cha muongozo wa usimamizi wa mali za umma, hafla iliyofanyika Ofisi ya Msimamizi wa hazina Maisara Mjini Unguja.

 

Msajili wa Hazina wa Serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar Waheed Sanya akisaini kitabu cha muongozo wa usimamizi wa mali za umma wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho huko Ofisini kwake Maisara Mjini Unguja.

 Msajili wa Hazina Zanzibar Waheed Sanya akitoa ufafanuzi kuhusu kitabu cha muongozo wa usimamizi wa mali za umma wakati akizindua kitabu hicho huko Ofisini kwake Maisara Mjini Unguja.

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...