Na MWANDISHI WETU


SERIKALI kupitia Bohari ya Dawa (MSD), imekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya sh milioni 900 kwa Halmashauri ya Ifakara mji.

Akizungumza jana Mkoani humo Mbunge wa Kilombero Abubakar Asenga, alisema ujio wa vifaa hivyo, utasaidia kuboresha huduma za afya hivyo wanaishukuru serikali kwa hatua kubwa ya maboresho katika sekta hiyo.

Alieleza kuwa, jimbo hilo lilikuwa na kero saba muhmu na kubwa ambazo hazijawahi kutatuliwa tangu kupata Uhuru lakini Rais Dk. Samia amezitatua ikiwemo mradi wa ujenzi wa barabara, maji, ukarabati kituo cha umeme Kidatu,ujenzi wa shule za kata, vituo vya afya, zahanati na hospitali.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kilombero Dunstan Kyobya amesema ujio wa vifaa tiba hivyo ni neema kwa halmashauri hiyo.

Alisema, maboresho hayo makubwa yanayofanywa na Rais Dk.Samia ni lazima kuungwa mkono na watendaji hivyo anatoa siku 15 kuhakikisha MSD inafunga vifaa hivyo na wananchi wanaanza kupata huduma.

“ Niwaombe MSD ilete wataalamu wao kwa ajili ya kufunga vifaa hivi, haiwezekani Rais wetu afanye mambo makubwa kama haya watendaji tumuangushe, ni muhimu kuhakikisha tunasimamia na wananchi wanaanza kupata huduma kwa wakati,”alisema.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa MSD ambaye ni Mfamasia na Afisa Huduma kwa Wateja Kanda ya Dar es Salaam Diana Kimario, alisema kanda hiyo ina hudumia mikoa mitatu ambayo ni Pwani, Morogoro na Zanzibar ambapo Ifakara ni mnufaika.

“Ujio wa vifaa hivyo vyenye thamani ya sh. milioni 900 ni muendelezo wa mabadiliko makubwa katika maboresho sekta ya afya, sisi watumishi ndani ya MSD tunajivunia namna serikali yetu chini ya Rais Dk. Samia na Mkurugenzi wa bohari Mavere Tukai wanavyohakikisha tunafanya kazi bila hofu.












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...