kutakuwa na mchezo wa soka mashindano ligi ya NBC baina timu ya Simba na Yanga zote za Jijini Dar es Salaam . Mchezo huo utaochezwa saa 11 jioni.

Jeshi la Polisi linatambua mchezo huo utakuwa na mvuto wa hali ya juu, hivyo kutakuwa na mkusanyiko mkubwa wa mashabiki wa soka wa timu hizo katika kiwanja hicho kutokana ushindani wa timu hizo. Kwa kulitambua hilo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama limechukua tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya mchezo huo.Ukaguzi wa hali ya juu utafanywa katika milango ya kuingia na hairuhisiwa mtu yeyote kwenda uwanjani na silaha ya aina yoyote, isipokuwa baadhi ya vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo hilo.

Asiyekuwa na tiketi hataruhusiwa kusogelea uwanja huo au maeneo ya milango ya kuingia. Tahadhari zote za kiusalama zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na baadhi ya barabara chache kufungwa ili kupunguza msongamano wa kuelekea na kutoka uwanjani siku hiyo. Jeshi linashauri mashabiki wa soka wafike mapema ili kuepusha usumbufu wa kuingia uwanjani kwani milango ya uwanja huo itafunguliwa kuanzia saa nne (4) asubuhi.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawatahadharisha baadhi ya mashabiki wenye tabia chafu zisizo za maadili kujiepushasha nazo kwani majukwaani watakuwepo makachero ambao watakuwa wakifuatilia kwa karibu vitendo vyote vya hovyo na baada ya mchezo watakaohusika na makosa hayo watakamatwa ili kukomesha tabia ambazo sio za kistarabu kwenye viwanja vya soka. Jeshi la Polisi linawatakia mashabiki wa soka na timu zao kila kheri.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...