Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
TANZANIA inategemewa kuwa wenyeji wa tuzo za Pacesetters (PSA) awamu ya nane mnamo Disemba 15 2023. PSA ni tuzo zinazolenga kusherehekea viongozi wakuu wa sekta kwa uvumbuzi wao, bidhaa bora, utoaji wa huduma, uundaji wa nafasi za kazi, uongozi wa mfano, kukuza uchumi, na kubadilisha jamii.
Kwa mujibu wa Jubilant Steward of Africa, waandaji wa tuzo hizi kampuni zaidi ya kumi (10) kutoka Tanzania zitawania ikiwemo Benki kuu za Tanzania, CRDB,NMB ,Raphael Logistics Limited Tanzania, Simba Logistics Equipment Supply Ltd Tanzania, Tanzania's Brett and Baileys Limited, Jambo Freight Limited Tanzania, Hyundai Tanzania, Spik and Span Limited Tanzania. na Inter Consult Limited Tanzania aidha kampuni shindani kutoka nchini zingine ni pamoja na Triple A Petroleum Ltd Sudan Kusini, Pembe Flour Mills Ltd, Wazalishaji wa Kavagara na Raha Premium Flour - Joy Millers Ltd Westlands Laser Eye Hospital, Safi Learning Zambia, Trinity Buses Rwanda, Ena Coach Kenya, Bryan Morel Publications Uganda, Digit Vehicle Tracking Uganda, Shantui,Sunflower Events Ltd Kenya, Ena Coach, Maasai Cables Limited, Mwananchi Credit Limited, Regional Leasing firm Vehicle and Equipment Leasing Ltd (VAELL), Rentco Africa, German Institute of Proffesional Studies, International College of Peace Studies.
Aidha washindi wa PSA wanapatikana kwa uangalifu kupitia mchakato wa ushindani na wa kina unaohusisha kura ya umma na jopo la majaji.
AISU ISAAC GODWIN, Mkurugenzi wa Jubilant Steward of Africa - Uganda alisema kuwa moja ya kazi kubwa ya shirika lao ni kuifanya jamii kuwa bora kwa kila mtu kwa kuhimiza makampuni kuendelea kufanya kazi nzuri ili yaweze kuendelea kuifanya nchi kuwa bora zaidi. Alifurahishwa na ujio wa mwaka jana na akasema alikuwa anatazamia tukio kubwa na bora zaidi mwaka huu.
Akizungumzia Tuzo hizi za Pacesetters Continental awamu ya 8, Bw. HASNAIN MENGHI, Mkurugenzi wa Masuala ya Kimataifa katika United SMES Association of Kenya alisema, “Tunafuraha kushirikiana na waandaaji wa Tuzo za Pacesetters na tunatazamia kuwaenzi wajasiriamali na taasisi za juu - Mashariki, soko la Afrika kwa juhudi zao za kuboresha uchumi na kuathiri maisha. Hii itahimiza mashirika na watu binafsi kwenda zaidi ya wito wa wajibu katika huduma yao kwa ubinadamu”
Jubilant Steward of Africa, ni Shirika Lisilo la Kiserikali linalotetea uboreshaji wa viwango vya maisha, maadili ya kijamii, utu na uwezeshaji wa jamii. Kama sehemu ya Uwekezaji wa Mashirika ya Kijamii (CSI), Jubilant Steward of Africa uwezesha na kuunga mkono makampuni na wataalamu katika azma yao ya kuboresha jamii na kuathiri maisha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...