Utekelezaji wa Miradi ya Utafiti inayohitaji utaalam ni muhimu ikaandikwa kwa ushirikiano baina ya watafiti mbalimbali wakiwemo wa ndani na nje ya nchi ili kuongeza Tija na uwezekano wa kupata ufadhili zaidi ya hayo ni kufanya Tafiti zitakazo zalisha matokeo bora.
Hayo yameelezwa na Prof. Japhet Kashaigili ambae ni Mratibu wa Utafiti na Machapisho kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Mshindi wa zawadi ya Mtafiti bora wa Chuo kwa mwaka 2022/2023 wakati akizungumza na wanahabari kwenye Mkutano wa Majalisi SUA ambao uliambatana na utoaji wa Tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo yao na watafiti katika Tafiti na kukiletea tija Chuo hicho.
Prof. Kashaigili amesema Mradi ambao ameuleta chuoni hapo unahusu maswala ya Mabadiliko ya Tabianchi na Ustahimilivu katika Nyanda Kavu za Kitropiki kuboresha upatikanaji wa maji Jijini Dodoma hivyo ni mkubwa kwakuwa umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 2.4 ukilinganisha na mingine ambayo ipo.
Aidha Prof. Kashaigili amesema Mradi huo umeweza kuwepo na kuonekana kuleta Tija kutokana na ukubwa wake yote hiyo ni kwasababu ya ushirikiano uliopo katika utekelezaji wa Mradi huo ambao umeshirikisha Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Taasisi mbalimbali za Uingereza, India na Afrika Magharibi ambapo kwa ujumla zipo Taasisi nane kwaajili ya utekelezaji wa Mradi huo.
“Upataji wa zawadi nikiwa kama Mtafiti bora wa Chuo ambae nimefanya Tafiti au Miradi ambayo imeonekana kukiletea heshima Chuo lakini pia kukiongezea kipato kwangu limekuwa ni jambo la fahari sana kwasababu kuna watafiti wengi hapa chuoni lakini nimeonekana mimi” alisema Prof. Kadhaigili
Kwa upande wake Prof. Robinson Mdegela ambaye pia alipata tuzo ya Mtafiti bora wa mwaka 2023 kutoka Ndaki ya Tiba ya Wanyama na Sayansi Shirikishi SUA amesema amefanikiwa kupata tuzo hiyo baada ya kufanya tafiti yenye kugusa maisha ya watanzania ikiwemo kupambana na ongezeko la usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa tatizo linalokaribia kuua watu karibu 12500 kwa mwaka kiwango ambacho ni karibu mara 10 ya idadi inayosababishwa na malaria au UKIMWI.
Amesema tangu ameanza kufanya tafiti SUA amefanikiwa kupata miradi zaidi ya 35 na kupeleka chuoni karibu shilingi Bilioni 23 kati ya hizo ameweza kutoa ufadhili kwa wanafunzi katika ngazi ya Uzamivu 57 na Umahiri 79 sambamba na kuchapisha majarida 2500.
“Kwa mwaka jana nilipata zawadi ya kuwa mtafiti bora niliechangia kupata fedha nyingi chuoni ambazo mwaka huu nimezitumia katika kufanya tafiti na kusaidia wanafunzi kupata ufadhili wa kufanya masomo yao katika ngazi mbalimbali za elimu zao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...