*Wakandarasi na wa watoa huduma 42 wapatiwa kazi

Dodoma
IMEELEZWA kuwa ujenzi wa Mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga unashirikisha wakandarasi wazawa kutoka mkoani Kagera.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga, kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko wakati alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu kutoka mkoani Kagera Mhe. Neema Kichiki Lugangira aliyetaka kujua je ni wakandarasi wangapi kutoka mkoani Kagera wamepata kazi katika mnyororo wa ujenzi wa bomba la mafuta la Hoima mkoani Tanga.

Mhe. Kapinga amesema kuwa wakandarasi wakuu wa Mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga wanaendelea kushirikiana na wakandarasi wadogo, wajenzi na na wanna huduma mbalimbali katika mikoa yote inayopitiwa na Mradi.

Mhe. kapinga aliongeza kuwa jumla ya wakandarasi na watoa huduma 42 wamepata kazi mbalimbali katika mnyororo wa thamani wa ujenzi wa Mradi huu ikiwemo uuzaji wa vifaa vya ujenzi, huduma za usambazaji wa mafuta, huduma za umeme na hoteli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...