Njombe
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Njombe imezidi kujiimarisha kiuchumi kupitia vyanzo vyake vya mapato ikiwemo milango iliyokodishwa kwa ajili ya maduka iliyopelekea kufikia makusanyo ya Shilingi Milion 201.6 kwa mwaka.
Akizungumza wakati akiaga wanachama wa Jumuiya hiyo na Chama cha Mapinduzi kwenye kikao cha baraza la la jumuiya hiyo kilichofanyika mjini Makambako Bi.Sauda Suleiman aliyekuwa katibu wilaya ya Njombe ambaye kwa sasa amehamishiwa katika wilaya ya Makete amesema alifika wilayani Njombe miaka mitatu iliyopita ambapo alikuta makusanyo ya shilingi Milioni 95 kwa mwaka.
"Nimekuta Milioni tisini na tano kwa mwaka lakini sasa hivi tuna Milioni mia mbili na moja laki sita na sabini na tano hii yote ni kwasababu nimefanya kazi kwa ujasiri na ninaondoka nikiwa najua Njombe ni salama,sikuikuta nyumba ya mtumishi lakini sasa ipo nyumba ya viwango na kwa kushirikiana na kamati tumepata tena nyumba ya kubwa ya kupangisha hapa Makambako"amesema Sauda
Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT wa wilaya hiyo Betrece Malekela amesema ni wajibu wa kila kiongozi kuweka alama wakati wa uongozi wake kwa kuweka miradi itakayoukuza uchumi wa Jumuiya huku katibu wa CCM wilaya ya Njombe Sure Mwasanguti akiwatahadharisha wanaoendelea kujipitisha na kufanya vitendo visivyo vya kiungwana kwenye kata na majimbo wakati viongozi wapo ambapo amesema Chama hicho kitakwenda kuwakata majina yao wote watakaobainika.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...