Njombe

Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amesema serikali ya mkoa huo inakwenda kuzungumza na wazazi wapya ili wajue nini maana ya kuwa mzazi lengo ikiwa kupunguza udumavu pamoja na vitendo vya ukatili mkoani humo.

Mtaka amebainisha hayo mkoani humo kwenye kikao cha uongozi wa mkoa kilichokuwa na lengo la kujadili mpango madhubuti juu ya udhibiti ugonjwa wa malaria na ugawaji wa vyandarua 45,107 kwa wanafunzi wote wa shule za msingi kuanzia darasa la kwanza mpaka la sita kwa halmashauri mbili za wilaya ya Ludewa na Njombe ambazo zinaongoza kwa maambukizi ya malaria mkoani humo.

Amesema vijana ndio wenye changamoto kubwa wanapoambiwa wamesababisha mimba hali inayosababisha kukataa ujauzito kwa madai ya kuto kujiandaa bila kujua hali hiyo ndio inayosababisha ukatili mkubwa.

"Hawa (vijana) ndio wanaopata changamoto na mabinti ujauzito ni wa kwako aaa! mimi sijajiandaa mtoto amebaki ametelekezwa kwa hiyo tunataka tuongee na hawa wazazi wapya ili ajue namna ya kuwa mzazi ni nini"amesema RC Mtaka





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...