Na Francisca Swai, Mahakama – Musoma

Jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, wamesikiliza jumla ya mashauri 32 ya Rufaa katika kikao cha Mahakama hiyo, kilichofanyika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma, kwa muda wa siku 19 kuanzia tarehe 30 Novemba, 2023 hadi tarehe 19, Novemba 2023.

Jopo la Majaji hao, linaongozwa na Mhe. Jaji Mwanaisha Kwariko, ambaye ni Mwenyekiti, Majaji wengine ni Mhe. Jaji, Zephrine Galeba na Mhe. Jaji, Dkt. Paul Kihwelo, ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto(IJA) kilichopo jijini Tanga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Rashid Chaungu alisema, katika mashauri 32 yanayoendelea kusikilizwa, mashauri 24 ni ya rufaa za Jinai na mashauri nane ni rufaa za Madai.

Mhe. Chaungu aliongezea kusema, hadi kufikia Novemba Mosi, 2023, jumla ya mashauri 19 yalikuwa yamesikilizwa.

Aidha, pamoja na usikilizwaji wa mashauri hayo kuendelea, Majaji hao, walivutiwana mandhari ya kuvutia ya bustani iliyopo katika maeneo ya Mahakama hiyo, Wahe. Majaji hao walipongeza juhudi zinazofanywa na uongozi wa Mahakama hiyo na kuhakikisha mazingira ya ndani na nje ya jengo hilo, yanakuwa katika hali safi na ya kuvutia.

Akipokea pongezi hizo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya, Mtendaji wa hiyo, Bw. Festo Chonya na Kaimu Naibu Msajili wake, Mhe. Erick Marley, walisema utunzaji wa mazingira ni moja ya kipaumbele muhimu katika Ofisi, licha ya uwepo wa changamoto za hali ya hewa, bado jitihada kubwa na usimamizi wa karibu unafanywa kuhakikisha mandhari nzuri iliyopo haipotei.

Katika ukaguzi huo, Majaji hao walifanikiwa kuona miti iliyopandwa na viongozi mbalimbali wa Mahakama ya Rufani Tanzania, akiwemo Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, Jaji Mhe. Ferdinand Wambali, Jaji Mhe.Ignas Kitusi, Jaji Mhe.Zephrine Galeba, Jaji Mhe.Lilian Mashaka,Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Manyara, Mhe. John Kahyoza, wengine ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Ephery Kisanya na Naibu Msajili wa Kituo cha Uboreshaji wa Huduma za Mahakama ya Tanzania, (JDU) Mhe. Mary Moyo.


Majaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Mwanaisha A. Kwariko (Katikati), Mhe. Dr. Paul F. Kihwelo (wa pili kulia) pamoja na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma Mhe. Fahamu Mtulya (wa pili kushoto), Mtendaji wa Mahakama Kuu Musoma Bw. Festo Chonya (wa kwanza kulia) na Kaimu Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma Mhe. Erick Marley (wa kwanza kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ukaguzi wa jengo na mazingira ya bustani Mahakama Kuu Musoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...