Na Mwandishi Wetu

WANAFUNZI wa shule ya msingi Hazina ya Magomeni jijini Dar es Salaam wameonyesha vipaji vya aina yake walipokuwa kwenye mahafali ya darasa la saba na shule ya awali.
Wanafunzi hao walionyesha vipaji kama kuimba, kucheza, sarakasi na mitindo mbali mbali ya mavazi hali ambayo iliwafurahisha wazazi walioshuhudia mahafali hayo.

Mkuu wa shule hiyo, Omari Juma alisema shule hiyo imekuwa na program ya michezo kwaajili ya kuangalia vipaji mbalimbali vya wanafunzi.

Alisema michezo mbali na kuimarisha afya za wanafunzi lakini inaweza kusaidia kwa wale wenye vipaji kuwa chanzo cha mapato kama baadhi ya wasanii waliofanikiwa.
Alisema Hazina itaendelea kuibua na kulea vipaji vya wanafunzi ili viweze kuwasaidia kwenye maisha yao ya kila siku kwani upo ushahidi wa watu waliofanikiwa kutokana na vipaji vyao.

“Kuna mwanafunzi mwingine anaweza kuwa wa kawaida darasani lakini akawa na kipaji kikubwa sana ambacho akikiendeleza anakuja kuwa msanii mkubwa sana na anaingiza fedha nyingi kwa hiyo utaratibu wa kuibua vipaji uwe endelevu kwa shule nyingi,” alisema Omari

Mmoja wa wazazi wa waliohudhuria mahafali hayo, Asha Aboubakary alipongeza shule hiyo kwa kuendesha program ya kuibua vipaji vya wanafunzi kwani wamejionea wenyewe namna wanafunzi walivyoonyesha umahiri kwenye sanaa.

“Kwa kweli tumeona wenyewe umahiri wa wanafunzi wa Hazina kwenye sanaa na mitindo mbalimbali kuanzia sarakasi, mitindo ya mavazi, kuimba na kucheza kwa hiyo vipaji huwa vinalelewa tumeona vipaji vingi ka hiyo wavilee vinaweza kuja kuwasiaida hawa watoto,” alisema






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...