Na Janeth Raphael -Dodoma
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kufanya zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga Kura katika Vituo 16 vya kuandikisha wapiga kuanzia Tarehe 24 -30 November 2023 ikiwemo Kata ya Ng'ambo iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Mkoa wa Tabora ,na Kata ya Ikoma iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Mkoani Mara.
Taarifa hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi RAMADHAN KAILIMA wakati akizungumza na Waandishi wa Habari na kusema lengo ni kupima uwezo wa Vifaa na Mifumo ya uandikishaji itakayotumika wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura unaotarajiwa kufanyika nchi nzima kwa tarehe na ratiba itakayopangwa na Tume.
Aidha uboreshaji wa majaribio utahusisha kuandikisha Raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea ,pia wapiga kura wanaoboresha taarifa zao ambao wamehama kutoka eneo moja la uchaguzi kwenda eneo jingine,walipoteza kadi au zilizoharibika , wanaorekebisha taarifa zao pamoja na kuondoa wapiga kura waliopoteza sifa za kuwemo katika Daftari.
Aidha Kailima amesema kuwa mfumo wa uandikishaji uliboreshwa utawezesha wapiga kura ambao wameshaandikishwa na wapo kwenye daftari la wapiga kura kuboresha taarifa zao au kuwasaidia kubadilisha kituo cha kupiga kura iwapo amehama Wilaya au Mkoa.
Katika hatua nyingine Kailima amesema kuwa uboreshaji wa majaribio hayo vyama vya Siasa vitashiriki kwa kuweka wakala mmoja katika kila kituo cha kuandikisha wapiga kura kwa lengo la kushuhudia na kujiridhisha kuhusu taratibu zitakazotumika wakati wa uboreshaji wa majaribio wa Daftari hilo.
Katika zoezi hilo Tume itatumia BVR Kits zenye vifaa mbalimbali vinavyowasiliana ili kuchukua na kutunza taarifa za Mpiga kura ,BVR Kits hizo zimeboreshwa na ni tofauti na zilizotumika katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura mwaka 2015 na 2019.
Hata Hivyo Tume hiyo imetoa wito wa wananchi wilaya hizo kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uboreshaji wa majaribio wa Daftari na kutoa ushirikiano kwa Tume ili kurahisisha utekezaji wa jukumu hilo kwa mustakabadhi wa Taifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...