WADAU nchini wametakiwa kutumia mbinu za kitaaluma zinazotokana na tafiti mbalimbali zinazofanywa katika kukabiliana na utumwa wa kisasa na usafirishaji haramu wa binadamu hali itakayosaidia kuepuka madhara yake kiuchumi pamoja na kijamii

Rai hiyo imetolewa hii leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Albert Chalamila wakati akizindua Kongamano la kimataifa linalolenga kujadili athari za utumwa wa zamani katika historia ya Afrika ya kisasa lililoandaliwa na Idara ya historia ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam lengo likiwa kujafili athari za utumwa katika maisha ya sasa barani Afrika.

Vilevile ameeleza kuwa bado kumekuwa na matukio kadhaa yanayohusisha utumwa na usafirishaji haramu bmwa binadamu hususa ni katika mkoa wa dar es salaam ambapo ameweka wazi kuwa jiji hilo limejidhatiti kukomesha suala hilo ikiwa ni pamoja na kutumia mapendekezo yatakayotokana na kongamano hilo.

Kwa upande wake Mhadhiri Mwandamizi idara ya historia na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo Dkt. Salvatory Nyanto amesema kongamano hilo limelenga kuja na njia za kukomesha utumwa wa kisasa ikiwa ni pamoja na kufanya majadiliano yatakayowezesha utungwaji wa sera na miongozo ya kukomesha biashara hiyo.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...