Na Mwandishi Wetu, Mkuranga

WAFANYABISHARA wilayani Mkuranga na Kibiti, wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuliza dhoroba ya hali ya biashara nchini.

Wamesema kwenye wilaya hizo biashara zinafanyika kwa amani na utulivu bila usumbufu tofauti na miaka ya nyuma.

Wametoa pongezi hizo kwa nyakati tofauti kwenye mkutano kati ya wafanyabishara wa wilaya hizo na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara (JWT) inayoendelea mkoani Pwani yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wafanyabishara.

Mfanyabiashara Hassan Mbwana Kambangwa, amesema wafanyabiashara kwa asilimia kubwa wilayani humo wananufaidika sana tangu kuingia kwa utawala wa Rais Samia.

Amesema "Kimsingi namshuruku Rais Samia kwa kutuletea ugeni uliotupa fursa ya kuzungumza changamoto zinazotukabili, lakini sisi tangu kuingia kwa utawala huu wa Mama Samia tunafaidika nao kwa asilimia kubwa."

Mfanyabiashara huyo ametolea mfano wa mambo wanayofaidika nayo kuwa ni mikopo, uhusiano mazuri na halmashauri lakini pia taasisi mbalimbali za kifedha ziko huru kuwasaidia wafanyabiashara.

Amesema serikali imezingatia suala la amani na utulivu na kwa mikoa mingi ilikua inapata changamoto nyingi lakini hapa wilaya ya Mkuranga wafanyabiashara wako huru na wanafanyabiashara bila bugudha.

"Tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan tunafanyabiashara kwa amani lakini pia tunashukuru ujio huu wa leo umefanya tuweza kufunguka yale ambayo yako ndani ya moyo na tunaamini mtayafikisha," Kambangwa.

Naye mfanyabishara Wilaya ya Kibiti, Salim Juma, amempongeza Rais Samia kwa kuona sekta ya wafanyabishara ni sehemu ya uchumi wa Taifa na kuamua kuungana kwa pamoja kutatua kero zao.

"Ili kuwa na ustawi tumefanikiwa kumpa Rais Samia, ambaye ameona umuhimu wetu na kutambua mchango wetu ndio maana leo viongozi mpo hapa," amesema Juma.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...