
Mkurugenzi Mkuu wa FCC, William Erio akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wamiliki wa viwanda na wafanyabiashara.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania CTI Bw. Leodgar Tenga akizungumza wakati wa mafunzo hayo kwa wafanyabiashara Wenye Viwanda nchini.



Na Cathbert Kajuna - MMG/Kajunason.
Tume ya Ushindani ya Tanzania (FCC), imewataka wafanyabishara na wamiliki wa viwanda nchini kutoa taarifa za kuwafichua watu wasio waaminifu ambao wanaingiza na kutengeneza bidhaa bandia kwani zinapoteza uchumi na kudidimiza pato la taifa.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), William Erio wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wamiliki wa viwanda na wafanyabiashara.
Amesema uwepo wa bidhaa bandia nchini kuna athari kubwa ikiwemo kuondoa ushindani sokoni na kupoteza mapato.
Erio aliwataka wafanyabishara na wamiliki hao wa viwanda kuchangamkia fursa ya soko huru la Afrika ambapo Tanzania ni miongoni mwa wanachama katika soko hilo la Afrika lililofunguliwa hivi karibuni wafanyabiashara watapata faida zaidi kwa kuuza na kutangaza biashara zao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa udhibiti wa bidhaa Bandia wa FCC, Khadija Ngasongwa amesema kuna athari kubwa za matumizi ya bidhaa hizo kwani faini zake ni kubwa kwa wale wanaobainika kuhusika lakini zinapoteza pato la taifa na kudidimiza uchumi.
Nae Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Bw. Leodgar Tenga amewashukuru FCC kwa kutoa mafunzo ambayo yanakwenda kuwajengea uwezo katika shughuli zao za uzalishaji.
"Binafsi nimefurahishwa sana na mafunzo mliyoyatoa maana yanakwenda kuwajengea uwezo hawa wamiliki wa viwanda," alisema Tenga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...