Na Vero Ignatus,Arusha

Wataalamu wanaotoa huduma za Afya mkoani Arusha wametakiwa kutoa huduma bora na stahiki kwa kwa wagonjwa,ilimkuhakikisha kuwa wanapona na kufikia lengo serikali la kupunguza idadi ya vifo visivyo vya lazima haswa kwa wakina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.

Ameyasema hayo mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella katika ziara ya kikazi wakati akikagua dawa na vifaa tiba, vilivyoletwa na serikali ,ikiwa ni baada ya kukamilika asilimia kubwa ya majengo kwenye Hospitali mpya ya wilaya ya Longido,mkoani hapa

Mongella aliwataka watoa huduma hizo za Afya kufanya kazi kwa weledi kwa ya kuwahudumia wagonjwa kwani serikali imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu pamoja wa ununuzi wa vifaa tiba,hivyo amewataka kuzingatia nia ya serikali ya kuweka miundombinu sahihi,hivyo hawanabudi kutimiza wajibu wao kwasababu wamepewa dhamana muhimu ya maisha ya watu

"Mhe Rais anahangaika kutafuta fedha, fedha ambazo zimetolewa kujenga hospitali hii pamoja na dawa na vifaa tiba, hakikisheni kila mtumishi anatimiza wajibu wake ili wananchi wavutike kutumia huduma kwenye hospitali zetu za serikali, haiwezekani mwananchi ateseke wakati serikali yake imeshaandaa miundombinu bora ya kumpa huduma bora, hivyo ni jukumu lenu kutimiza wajibu wenu ili kufikia lengo la serikali kwa kuwa mmepewa dhamana hiyo muhimu ya maisha ya watu''Alisema Mongella

Alisema kuwa endapo wahudumu hao watatoa huduma bora watawapunguzia wananchi gharama za kwenda hospitali ya Mount Meru sambamba na punguza msongamano wa wagonjwa waliokuwa wanafuata huduma hospitalini hapo kwani serikali inahitaji kila mwananchi apate huduma zote ndani ya eneo analoishi jambo ambalo litapunguza gharama nakuongeza utunzaji wa muda kwa wananchi wa kutafuta huduma za afya mbali.

Aidha hospitali hiyo inategemea kuhudumia zaidi ya wagonjwa 175,915 wa wilaya ya Longido na wengine kutoka Nchi jirani ya Kenya, kukiwa na lengo la kutoa huduma zote za afya pamoja na kupungumza gharama kwa wagonjwa kusafiri mpaka Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru jijini Arusha, sambamba na kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali hiyo ya Rufaa.

Akifafanua juu ya mradi kuwa huo amesema kwa asilimia kubwa umetekelezwa na Serikali kwa gharama ya shilingi Bilioni 3.4, ambapo shilingi Bilioni 3 ni fedha kutoka Serikali kuu huku shilingi milioni 340 ni kupitia fedha za mapambano dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO 19.

Ikumbukwe kuwa ujenzi wa hospitali za wilaya ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM wa kuhakikisha kila Wilaya inakuwa na Hopitali kwa lengonla kusongeza huduma muhimu karibu na wananchi ikiwa na mapngo maalum wa kupambana na kuzuia vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella akizungumza na wahudumu mara baada ya kuwasili katika hospitali nya wilaya ya Longido ikiwa ni mmoja ya ziara yake ya kikazi.

Mkuu wa mkoa wa Arusha akiangalia mmoja ya vifaa katika hospitali ya wilaya ya Longido


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...