Katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella akiteta na watendaji katika wilaya ya Longido alipokuwa katika ziara ya kikazi,ambapo aliweza kukagua mradi wa shule mpya ya sekondari ya Sinya .
Moja ya jengo la madarasa katika shule mpya ya Sinya katika halmashauri ya wilaya ya Longido
Muonekano wa mkukamilika kwa matundu ya choo katika sule mpya ya sekondari Sinya wilayani Longido
Na Vero Ignatus, Arusha.
Mradi unaotekelezwa na Serikali kwa gharama shilingi milioni 470 fedha kutoka Serikali kuu kupitia mpango wa kuboresha Miundombinu ya Serikali nchini (SEQUIP)majengo yamekamilika kulingana na gharama ya fedha zilizotolewa
Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa John Mongella kuwa shule hiyo imesajiliwa kwa namba SINYA S. 6298 inatarajia kupokea wanafunzi mapema Januari 2024 ambapo amewataka viongozi na watalam kila mmoja kwa nafasi yake kuwajibika na kuhakikisha miradi ya maendeleo inasimamiwa vema na kukamilika kwa wakati ili iweze kutoa huduma kwa wananchi.
Mara baada ya kutembelea na kukagua hali halisi ya mradi huo pamoja na muonekano wa majengo Mongella amesema ameridhishwa na mradi huo, kwani viwango vya ubora vinavyoendana na thamani ya fedha iliyotolewa na serikali awamu ya sita imetumika ipasavyo
Sambamba na hayo ameweza kuuponeza uongozi wa wilaya ya Longido, wakiwemo viongozi wa chama, baraza la Madiwani pamoja na Mwalimu msimamizi wa mradi huo ambaye ni mkuu wa shule ya sekondari Tingatinga kwa kazi nzuri ya usimamizi wa miradi pamoja na kufanikisha usajili wake.
"Miradi hii ya elimu inaposhindwa kukamilika kwa wakati, tunawakosea haki watoto wetu, serikali imetoa fedha za kukamilisha miradi, jukumu lenu ni kusimamia ili ikamilike kwa wakati na watoto wapate haki yao ya msingi".Amesema Mongella.
Awali akiwasilisha Taarifa ya mradi huo, Mkuu wa shule sekondari Tingatinga Pantaleo Pareso amesema kuwa, milioni 470 zimejenga vyumba 8 vya madarasa, jengo la utawala, jengo la Maabara, chumba cha TEHAMA, matundu 16 ya vyoo, ununuzi wa matank ya kuhifadhia lita 1000 za maji
Hata hivyo wananchi wa kata ya Sinya, wameishukuru serikali kwa ujenzi wa shule hiyo mpya, shule ambayo licha ya kukata kiu yao ya muda mrefu, itawapa fursa watoto wao kusoma karibu na nyumbani.
Mwenyekiti wa UWT kata ya Sinya, Norkishumu Otuma Sakita, amesema kuwa licha ya kuwa tulitamani kuwa na shule ya sekondari lakini hatukuwahi kuwaza kuwa na shule kama tutapata shule mapema, mama Samia ametukumbuka sisi wamama, watoto watapata elimu ya sekodnari na kwenda chuo kikuu kama watoto wengine.
Naye Nangakiwa Gwarugulito, amemshukuru Rais, Dkt.Samia kwa kuwajengea shule kijijini kwao, walikuwa na shule ya msingi tu, walitumia gharama kubwa kuwapelekea watoto shule za mbali, lakini sasa wamepata shule nyumbani.
"Tunaamini kwa sasa watoto wetu watapata nafasi ya kusoma chuo kikuu, watoto wetu watakuwa wasomi na kuwa viongozi wa kubwa wa nchi hii, kijiji chetu kitakuwa na wasomi sasa" Amesema Nangakiwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...