Benki ya Letshego Faidika imezidi kuwawezesha wateja wao kupitia kupitia kampeni ya KOPA TUKUBUSTI ambapo wateja zaidi watano wamshindda fedha taslimu.

Wateja hao ni Chausiku Ndimila aliyeshinda Sh357,651, Abdurahman Mwambasi aliyeshinda Sh320,365 na Ngolo Mgeni aliyeshinda Sh 2 milioni.

Wateja wengine walioshinda ni Grace Yangi aliyeshinda Sh471,335 na Masanja Simeo aliyeshinda Sh134,635.

Wateja hao wameshinda kiasi hicho cha fedha baada ya kukoa fedha katika benki hiyo kupitia kampeni ambayo kwa sasa imeshika kasi ya KOPA TUKUBUSTI.

Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa benki ya Letshego Faidika Bw Asupya Nalingigwa washindi hao watano wanafikisha jumla ya washindi 25 tokea kuzindua kampeni hiyo.

Bw Nalingigwa amesema kuwa kampeni hiyo inamtaka mteja wao kukopa fedha taslimu na kuingia kwenye droo ambayo mshindi atapata asilimia 50 zaidi ya kiasi alichokopa.

Aliwapongeza washindi hao kwa kujipatia fedha hizo ambazo uwekwa kwenye akaunti ya mshindi moja kwa moja.

Bw Nalingigwa alisema kuwa kampeni hiyo inazidi kushika kasi na kuwaomba wateja wao kuchangamkia mikopo yao ili kushinda zawadi mbalimbali na kuweza kusaidia kugharimia mahitaji mbalimbali.

Benki hiyo imetenga kiasi cha Sh50 billion kwa ajili ya kuwazawadia wateja wao kupitia kampeni hiyo.

 “Lengo letu kubwa ni kuwawezesha wateja wetu na kuwek jumla ya Sh50 bilioni kwa ajili ya kuwakopesha. Kama tulivyosema awali, mteja anaweza kushinda fedha ya ziada (Bonus) ya asilimia 50 ya kiasi cha fedha alichokopa kupitia kampeni hii mpya ya KOPA TUKUBUSTI,” alisema. Bw. Nalingigwa.

Kwa mujibu wa Bw Nalingigwa, vigezo mbalimbali vimewekwa kwa washiriki wa kampeni hii ikiwa pamoja na umri kuanzia miaka 18, lazima awe mfanyakazi aliyethibitishwa wa serikali na taasisi binafsi na lazima awe na sifa za kupata mkopo kwa mujibu wa vigezo na masharti.

Mkuu wa Kitengo cha  Mauzo wa benki ya Letshego Faidika Bw Asupya Nalingigwa akisisitiza jambo wakati wa kuchezesha droo ya kampeni ya Kopa Tukubusti yenye lengo la kuwafaidisha wateja wa Benki Hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Benki ya Letshego Faidika Bw. Asupya Nalingigwa (katikati) akizungumza wakati wa droo ya kutafuta washindi wa kampeni ya Kopa Tukubusti yenye lengo la kuwafaidisha wateja wao. Kulia ni afisa wa kitengo cha teknolojia ya habari na mawasiliano wa kampuni ya Radian Limited  Kundani Makimu na kushoto ni Afisa Msimamizi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Pendo Mfuru.

Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Benki ya Letshego Faidika Bw. Asupya Nalingigwa (katikati) akizungumza wakati wa droo ya kutafuta washindi wa kampeni ya Kopa Tukubusti yenye lengo la kuwafaidisha wateja wao. Kulia ni afisa wa kitengo cha teknolojia ya habari na mawasiliano wa kampuni ya Radian Limited  Kundani Makimu. Wa kwanza kushoto ni Fay Musira ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko ya Kidigitali wa Kampuni ya Radian na wa pili kushoto ni Afisa Msimamizi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Pendo Mfuru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...