Na,Vero Ignatus,Arusha

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeutaka Uongozi na watumishi wa Chuo cha Utalii Kampasi ya Arusha (NCT)kimetakiwa kuwa na wabunifu katika kuandika maandiko yanayoendana na hali halisi ya biashara ya utalii Duniani, kwani kutakapokuwa na maandiko ya kisasa yanayoshawishi uboreshaji wa biashara ya utalii ndivyo tutakavyo kuza biashara ya utalii na kuongeza mchango wa pato la taifa kutoka katika Chuo cha Utalii Tanzania

Ameyasema hayo Naibu Waziri wa maliasili na Utalii Dunstan Kitandula wakati alipokuwa akiongea na watumishi wa chuo hicho kilichopo maeneo ya Sakina Jijini Arusha ambapo aliutaka uongozi wa chuo hicho kujipima au kujitathimini kwa kina namna ambavyo wataweza kubeba mzigo mkubwa kutokana na mikakati ambayo imejiwekea na makubaliano waliyowekeana na taasisi mbalimbali ambazo chuo cha Utalii kitandaa wataalamu wa ukarimu wa taasisi hizo

Aidha Kitandula aliongeza kuwa ili chuo hicho kiwe hai na kuonekana lazima kuwepo na maandiko ya kibiashara yanayoshawishi wafadhili au serikali kutoa fedha kwa ajili ya maendeleo ya chuo,vilevile amepongeza chuo hicho kwa jitihada na hatua mbalimbali wanazochukua katika kuhakikisha chuo kinatoa wahitimu walio bora na waliopata mafunzo kwa vitendo katika uhalisia wa biashara ya utalii inayoendela Duniani.

“Nawapongeza kwa ujenzi unaondelea katika eneo hili kwani kwa kufanya hivyo mtaongeza udahili wa wanafunzi katika fani mbalimbali zinazoendeshwa hapa chuoni” Alisema Mhe. Kitandula

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Utalii Tanzania, Dkt. Florian Mtei akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii kuzungumza, ameushukuru uongozi wa wizara unaoongozwa Mhe. Angellah Kairuki Waziri wa Maliasili na Utalii kwa kuwa umekuwa karibu na Chuo katika kusaidia mambo mbalimbali kwa ajili ya ajili ya Maendeleo ya Chuo cha Utalii Tanzania

Baadi ya wanafunzi wa Chuo cha Utalii Kampasi ya Arusha (NCT)kama wanavyoonekana katika picha
Wanafunzi wa Chuo cha Utalii Kampasi ya Arusha (NCT)wakimsikiliza Naibu Waziri wa maliasili na Utalii Dunstan Kitandula alipotembelea chuoni hapo kama wanavyoonekana katika picha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...