Na.Khadija Seif Michuziblog

KWAYA ya Uinjilisti Kanisa la KKKT Kijitonyama wa waalika waumini wa dini ya Kikristo na madhehebu mengine kushiriki tamasha la kuimba na Kusifu Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Wanahabari Leo Novemba 29,2023 Makamu Mwenyekiti Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama Everlight Matinga amesema Tamasha hilo la Kumtukuza na kumshangilia Mungu kwa ibada na nyimbo linafanyika tena kwa msimu wa 4 ambapo linatarajiwa kufanyika Disemba 03,2023 katika Viwanja vya Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.

Aidha ameeleza kuwa Tamasha hilo limekuwa likifanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na lengo hasa kubwa kutangaza injili kwa njia ya uimbaji na maombezi.

Hata hivyo ameeleza kuwa Tamasha hilo ni bure hakuna kiingilio.

Kwa upande wake Mlezi wa Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama Mstaafu Meja Reverian Mchwampaka amewaomba Watanzania wote kujitokeza katika tamasha hilo kwa ajili
ya Maombezi .

"Wote kutoka ndani na nje ya Dar es Salaam kwa pamoja na madhehebu mbalimbali nchini tuje kuiombea nchi yetu pamoja na familia zetu ."

Nae Muimbaji wa Kwaya hiyo Mathew Cathbert amefafanua zaidi kuwa Tamasha hilo litashirikisha Waimbaji kutoka Kwaya mbalimbali ikiwemo Kwaya ya Mtakatifu Kizito,Kwaya ya Jerusalem na wengi wengi kwa ajili ya kusherehesha tamasha hilo.

"Tamasha hili litashereheshwa na Kwaya yetu ya Uinjilisti Kijitonyama ambapo nyimbo takribani 09 zitatumbuizwa kwa vyombo yani mubashara na tumealikwa kwaya zingine ili tuweze kusherehekea Tamasha hili kwa ladha ya tofauti tofauti. "

 

Makamu Mwenyekiti wa Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama Everlight Matinga akizungumza na Wanahabari Leo Novemba 29,2023 wakati akitambulisha Tamasha la msimu wa 4 wa kwaya hiyo "Siku ya mbingu kujaa sifa " linalotarajiwa kufanyika mapema Disemba 02,2023 katika Viwanja ya Kijitonyama Jijini Dar es Salaam
 

Mlezi wa Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama Mstaafu Meja Reverian Mchwampaka akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa Tamasha la "Siku ya mbingu kujaa sifa" na Kuwataka Watanzania kuhudhuria katika Viwanja vya Kijitonyama Jijini Dar es Salaam
 

Mwakilishi upande wa Kwaya ya Uinjilisti Kanisa la KKKT Kijitonyama akifafanua zaidi jinsi walivyojipanga kutoa burudani mbalimbali na vibao vitakavyotumbuizwa siku ya Tamasha la "Siku ya mbingu kujaa sifa disemba 02,2023 Jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...