Na Imani Mtumwa , Maelezo

Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume Dk Mahmoud Alawi amesema mafunzo ya akili bandia ni muhimu kupatiwa wafanyakazi nchini ili kuendeleza Mapinduzi ya nne ya Viwanda.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uelewa watendaji wa taasisi mbalimbali juu ya teknoloji hiyo katika ukumbi wa Taasisi ya Karume Mbweni alisema kwasasa dunia inaelekea kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda ambapo matumizi ya roboti yatahitajika ili kurahisisha utendaji kazi.

Hivyo Mafunzo hayo yanaenda kuwajengea uwezo wafanyakazi hao kuweza kutumia roboti katika kurahisisha kazi zao.

Alisema akili bandia (roboti ) ina uwezo wa kufanya kazi nyingi kama binaadamu hivyo teknolojia hiyo itaenda kuisaidia Serikali hasa katika sekta ya viwanda kutekeleza majukumu yake kwa urahisi zaidi.

Awali dkt. Mahmoud aliwataka washiriki hao kuwa watulivu na kufuatilia mafunzo hayo ili kufikia malengo yaliokusudiwa.

Kwa upande wake Naibu Mkuu wa Taasisi Karume Taaluma Dkt. Khamis Khalid Said alisema kukamilika kwa mafunzo hayo kutasaidia kurahisisha utendaji katika maeneo mbali mbali ikiwemo ya Biashara, sekta ya Afya, Usafirishaji na Nishati.

Aidha alifahamisha kuwa mafunzo hayo yamefanyika kutokana na mashirikiano mazuri yaliopo kati ya Taasisi ya karume na Chuo cha AP cha Belgium kwa lengo la kupata ubunifu na kuboresha utendaji kazi.

Mkufunzi kutoka Chuo cha AP University Piric Ven Muoek amesema katika kuhakiksha mradi huo unafikia malengo wanafunzi wanne wa chuo hicho watapata fursa ya kuendeleza Mafunzo hayo nchini Belgium ili kuweza kuiendeleza programu hiyo Zanzibar.

Nao baadhi ya Washiriki akiwemo Mkuu wa programu za uwezeshaji Wakala wa uwezeshaji Wananchi kiuchumi ZEEA Raya Idrisa Ahmada wameseam Mafunzo hayo yanaweza kuleta mabadili ya kiutendaji Nchini na kuziomba taasisi zinazo husika na masuala ya Viwanda kutoa ushirikiano ili kuuendeleza mradi huo hadi kufikia malengo .

Mafunzo hayo ya siku 5 yaliwashirikisha wajasiriamali na watendaji wa taasisi mbali mbali za ndani na nje ya Nchi.

 

Mkuu wa TAASISI ya Sayansi na Teknolojia ya  Karume Dkt Mahmoud Alawi akifungua mafunzo ya kuwajengea uelewa watendaji wa taasisi mbalimbali  juu ya teknolojia ya akili mnemba (artificial inteligent),Hafla iliyofanyika katika taasisi hiyo iliopo Mbweni Zanzibar.
 

Naibu mkuu wa taasisi ya Karume Taaluma Dkt.Khamis Khalid Said akichangia mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa watendaji wa taasisi mbalimbali  juu ya teknolojia ya akili mnemba Hafla iliyofanyika Chuoni hapo Mbweni Zanzibar.

 

Mkufunzi kutoka Chuo cha AP University  Piric Ven Muoek akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa watendaji wa Taasisi mbalimbali  juu ya teknolojia ya akili mnemba Hafla iliyofanyika Chuoni hapo Mbweni Zanzibar.

 

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...