Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
WAZAZI
na walezi Mkoani Pwani wameaswa kujenga ukaribu kwa watoto wao pamoja
na kuwapa haki ya kujieleza pale inapobidi ,ili waweze kufichua Yale
ambayo yanawakabili hasa kwenye vitendo vya unyanyasaji wa watoto.
Aidha
jamii imetakiwa kuhakikisha ulinzi na usalama wa mtoto kwa kumuondolea
vikwazo na kutoa taarifa kwa wanaofanya vitendo vya ukatili ili mtoto
aweze kutimiza ndoto zake.
Rai
hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani ,Rashid Mchatta
alipokuwa akizindua mradi wa Usalama wa Watoto (UWAWA) awamu ya pili
unaosimamiwa na Christian Social Services Commission (CSSC),ulioanza
2023 septemba na utakamilika 2026.
Mchatta
alieleza ,watoto wanakabiliwa na changamoto nyingi ambapo jamii
inatakiwa kusema na watoto wao na kuwalinda pasipo kuwa wakali.
"Mradi
huu wa UWAWA inaunga mkono juhudi za Serikali kuzingatia usalama na
haki kwa watoto, lengo ni kuimarisha usalama wa watoto" alifafanua
Mchatta.
Naye Ofisa elimu
Mkoa wa Pwani Sara Mlaki aliwataka wazazi kusimamia malezi ya watoto na
kufuatilia masomo yao bila kuwaachia walimu pekee.
Mlaki aliwataka wale wazazi wanaonyanyasa watoto wao waache na badala yake waongeze upendo kwao .
Alisema,
vitendo vya ukatili kwa watoto wakati mwingine vinatokana na utandawazi
ambapo amewasihi wasitumie mitandao ya kijamii kuonyesha vitendo vya
ukatili kwa watoto.
Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya Mashariki wa (CSSC) Makoye Wangeleja aliushukuru mkoa kwa kutoa ushirikiano.
Alieleza,vita
unyanyasaji na ukatili kwa watoto siyo lelemama ,watu wanaowafanyia
vitendo hivyo ni watu ambao huwezi kuwafikiri na inabidi kujipanga ili
kukabili vitendo hivyo .
Makoye
alieleza, wazazi wamekuwa wakikosa muda wa kukaa na watoto ,wanaachia
wadada wa kazi na walimu ,na wakirudi nyumbani wanashindwa kujenga
urafiki na watoto na kuwa wakali hata wakitaka kuelezwa Jambo.
"Hili
ni tatizo kubwa, unakuta mtoto anataka kujieleza,labda kaffanyiwa
vitendo vya ukatili,mzazi anamnyamazisha mtoto, unakuta mtoto anayasema
nje ya familia suala ambalo sio jema kwani wanakosa uhuru wa kuzungumza
na kujieleza" alieleza Makoye.
Ofisa
ustawi wa jamii Kibaha Mjini, Mary Michael alieleza chanzo kingine ni
wazazi kutelekeza watoto huku wakijikuta wakikosa malezi mema.
Aliomba
ushirikiano uwepo kwa ngazi za jamii, Serikali, madawati ya jinsia,
Jamii na wadau ili kukomesha vitendo vya kijinsia kwa watoto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...