Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetwaa Tuzo kwa kuwa mshindi wa kwanza kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa. NSSF imepokea cheti na tuzo hiyo kwa kutambua utendaji kazi wa hali ya juu katika Wiki ya Huduma za Fedha.

Wiki ya huduma za fedha hufanyika kila mwaka na inaratibiwa na Wizara ya Fedha ikishirikisha wadau wa masuala ya fedha nchini, ambao ni wizara na taasisi za serikali, mabenki, makampuni ya bima pamoja na wadau wengine wa serikali na sekta binafsi.

Kwa mwaka huu, Wiki ya Huduma za Fedha imefanyika jijini Arusha na ilianza tarehe 20 na inafikia tamati kesho tarehe 26 Novemba 2023.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...