Na mwandishi wetu,Kigoma

WATUMISHI 11 wa Manispaa ya Kigoma Ujiji pamoja na TAMISEMI wamepandishwa kizimbani wakikabiliwa na kesi ya Uhujumu uchumi namba 3 ya mwaka 2023 yenye mashtaka 11 likiwemo la utakatishaji fedha Sh.milioni 463.5

Akisoma mashtaka hayo mbele ya hakimu Mfawidhi wa mahakama
hiyo Hassan Momba,Wakili Mwandamizi wa Serikali Anosisye Erasto aliieleza mahakama kuwa washitakiwa walitenda makosa hayo kati ya Juni 1,  2022 na Juni 5 2023 katika Manispaa ya Kigoma ujiji na Jiji la Dodoma

Baadhi ya mashitaka wanayoshitakiwa ni pamoja na kula njama kwa nia ya kutenda koda,kugushi,matumizi mabaya ya madaraka,kutakatisha fedha,kuisababishia mamlaka ya serikali hasara.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma ujiji Athumani Msabila,watumishi wa ofisi ya Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Dodoma Aidan Mponzi na Tumsifu Kachira.

Watumishi toka ofisi ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Frednand Filimbi,Salum Juma,Moses Zahuye,Joel Shirima,Jema Mbilinyi,Kombe Kabichi,Frank Nguvumali na Bayaga Ntamasambilo kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.

katika kesi hiyo washitakiwa wanasimamiwa na mawakili wanne ambao ni Sadiki Aliki,Michael Mwangati,Eliutha Kvyiro na Victoria Nyembea.

Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutona na mahakama kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza mashauri yao ikiwemo shitaka la uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara.

Kesi hiyo imehairishwa had Novemba 20 mwaka huu itakapotatajwa tena kwaajili ya kutoa uamuzi wa dhamana kwa washitakiwa watano ambao hawahusiki na shitaka la utakatishaji fedha kama watakuwa na haki ya kupata dhamana.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...