Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo amewataka wawekezaji wa Biashara ya Kaboni nchini kuwa wawazi katika biashara hiyo.

Ametoa maelekezo hayo wakati wa hafla ya makabidhiano ya hundi ya malipo ya sh. bilioni 47 kwa wakazi wa Wilaya za Kiteto na Mbulu ambazo zimenufaika na mradi huo mkoani Manyara leo Novemba 14, 2023.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Jafo amewaelekeza wawekezaji kuwa na vyeti vinavyoonesha mahali walipouza bidhaa zao ili kuwa wawazi kwa mujibu wa kanuni ya 4 ya Sheria ya Mazingira inayowataka kuwa na uwazi katika biashara zao.

Kwa muktadha huo amewataka kuwa wawazi zaidi na mchanganuo unaoonesha mwanakijiji na mwekezaji wananufaikaje na Biashara ya Kaboni ambayo inachagiza uhifadhi wa mazingira kwa kupanda miti.

Hali kadhalika Waziri Jafo amefafanua kuwa biashara hiyo inafanyika katika masoko mbalimbali ya hisa, hivyo ameelekeza nitoe maelekezo kila mwekezaji kuweka wazi cheti kinachoonesha mahali alifanya biashara yake.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga amesema Kanuni za Biashara ya Kaboni zilizoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa rais zimesaidia kusimamia biashara hiyo.

Ameongeza kuwa fedha zitokanazo na biashara hiyo ya hewa ya zimewasaidia kuboresha huduma mbalimbali za kijamiii ikiwemo ujenzi wa zahanati, barabara na shule hivyo zimeisaidia jamii ya Wahadzabe kuwapeleka watoto wao shule.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Heri James ameelezea faida zilizopatikana kutokana na Biashara ya Kaboni kuwa ni kuchochea matumizi bora ya ardhi hivyo kupunguza migogoro ya ardhi.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga alipowasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi leo Novemba 14, 2023.
 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya hundi ya malipo ya sh. bilioni 47 kwa wakazi wa Wilaya za Kiteto na Mbulu ambazo zimenufaika na mradi huo mkoani Manyara leo Novemba 14, 2023.
 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. Bilioni 4.7 kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga kwa ajili ya wakazi wa Wilaya za Kiteto na Mbulu ambazo zimenufaika na Biashara ya Kaboni, leo Novemba 14, 2023.
 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo na viongozi mbalimbali wakionesha mfano wa hundi yenye thamani ya sh. Bilioni 4.7 aliyoikabidhi kwa ajili ya wakazi wa Wilaya za Kiteto na Mbulu ambazo zimenufaika na Biashara ya Kaboni, leo Novemba 14, 2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...