Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Mohamed Malick Salum kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC). Kabla ya uteuzi huu Bw. Salum alikuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Wizara ya Uchukuzi.
Bw. Salum anachukua nafasi ya Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC).
Uteuzi huu unaanza tarehe 14 Novemba, 2023.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...