NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, ARUSHA
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea banda
la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwenye Maadhimisho ya 3 ya Wiki ya
Huduma ya Fedha Kitaifa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha
Novemba 22, 2023, ili kujionea jinsi wanavyowahudumia wananchi.
Mhe.
Majaliwa alipokelewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana Ajira
na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhanisi Cyprian Luhemeja na
kupitishwa kwenye mabanda yaliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, WCF ikiwemo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, alimueleza Waziri Mkuu kuwa WCF na mifuko mingine ya hifadhi ya jamii, inashiriki katika Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo, "Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo Kiuchumi", ili kutoa elimu kwa umma kuhusu hifadhi ya jamii lakini pia elimu ya matumizi sahihi ya fedha.
Alisema,
WCF, inahudumia wafanyakazi wanaoumia au kuugua wawapo kazini.
“Ni
muhimu sana kwa waajiri kuwekeza katika afya za wafanyakazi kwani binadamu
anaweza kupatwa na changamoto wakati wowote na hapo ndipo unakuja umuhimu wa
waajiri kujisajili ili kuwawekea kinga ya kipato wafanyakazi wao wanapopatwa na
changamoto wanapotekeleza majukumu ya kazi walizoajiriwa kuzifanya.” Alisema.
Akieleza
kuhusu jinsi wanavyohudumia wananchi wanaotembelea kwenye banda hilo, Mkuu wa
Kitengo cha Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge, alimueleza Waziri Mkuu kuwa, wanatoa
elimu ya fidia kwa wafanyakazi, lakini pia Mafao yanayotolewa na Mfuko kwa
Mfanyakazi anayeumia au Kuugua kutokana na kazi na endapo atafariki, basi Mfuko unabeba jukumu la
kuwalipa fidia wategemezi wake.
“Kwa
hivyo kupitia mafao tunayotoa, tunapunguza umasikini katika jamii yetu.” Alisema.
WAZIRI
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (wapili kulia),
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe.
Profesa Joyce Ndalichako (wakwanza kulia), Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu
(Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu), Mhandisi Cyprian Luhemeja, (wapili
kushoto), wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
(WCF), Bi. Laura Kunenge, wakati akieleza huduma zitolewazo kwenye banda la
Mfuko huo Novemba 22, 2023.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...