Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameonyesha kuvutiwa na mchango unaoendelea kutolewa na benki ya Taifa ya Biashara (NBC) katika kukuza sekta mbalimbali nchini ikiwemo kilimo, biashara na michezo kupitia huduma na ufadhili wa benki hiyo kwenye maeneo hayo.
Waziri Mkuu Majaliwa alitoa pongezi hizo alipotembelea banda la benki hiyo lililopo kwenye viunga vya ukumbi wa Mkutano Mkuu wa saba wa mwaka wa Jukwa la Wahariri Tanzania (TEF), unaofanyika Mkoani Lindi. Benki ya NBC ni moja ya wadhamini muhimu wa Mkutano huo wa siku mbili.
Akiwa kwenye banda hilo Waziri Mkuu alipata wasaa wa kupata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo katika sekta mbalimbali ambapo alionyesha kuvutiwa na huduma ya NBC Shambani inayotolewa na benki hiyo mahususi kwa wakulima wakiwemo wakulima wa zao la korosho.
Waziri Mkuu Majaliwa pia aliipongeza benki hiyo kwa mchango wake kwenye sekta ya michezo hususani udhamini wake kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara yaani NBC Premiere League, Ligi ya Vijana pamoja na NBC Championship.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Kulia) akitazama baadhi ya vipeperushi kuhusu huduma zinazotolewa na Benki ya NBC huku akimsikiliza Meneja wa NBC tawi la Lindi Bw. Iovin Mapunda (Kushoto) akitoa maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo akaunti ya NBC Shambani mahususi kwa wakulima wakati Waziri mkuu alipotembelea banda la benki hiyo lililopo kwenye viunga vya ukumbi wa Mkutano Mkuu wa saba wa mwaka wa Jukwa la Wahariri Tanzania (TEF), unaofanyika Mkoani Lindi. Benki ya NBC ni moja ya wadhamini muhimu wa Mkutano huo wa siku mbili.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Kulia) akizungumza na baadhi ya maofisa wa benki ya NBC akiwemo Meneja wa NBC tawi la Lindi Bw. Iovin Mapunda (Kushoto) na Meneja Mahusiano wa beniki hiyo Bi Brendansia Kileo (Katikati) wakati alipotembelea banda la benki hiyo lililopo kwenye viunga vya ukumbi wa Mkutano Mkuu wa saba wa mwaka wa Jukwa la Wahariri Tanzania (TEF), unaofanyika Mkoani Lindi. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi Zainabu Telack. Benki ya NBC ni moja ya wadhamini muhimu wa Mkutano huo wa siku mbili.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...