Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George B. Simbachawene amewasisitiza Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu Tanzania kuendelea kutimiza malengo kwa kuzingatia maadili, nidhamu na uaminifu katika kufanya kazi na kukuza taaluma nchini.

Ameyasema hayo wakati  akifungua mkutano wa mwaka wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania uliofanyika jijini Dar es salaam ambapo Wahasibu na Wakaguzi zaidi ya 2000 kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi wamekutana kujadili mambo mbalimbali yanayohusu fani hiyo.

Amewasisitiza Wahasibu nchini kusimamia maadili ya Taaluma hiyo kwani ndio msingi mkubwa wa maendeleo hapa nchini pamoja na nchi nyingine hivyo wakienda kinyume watachukuliwa hatua stahiki ili kuweza kupunguza ubadhilifu wa fedha za Umma.

Bodi ya NBAA endeleeni kuwasimamia Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu vizuri na wakienda kinyume na maadili na viapo vyao msisite kuwachukulia hatua kwani mkifanya hivyo italeta funzo wa Wahasibu wengine.

 Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia S. Temu amesema kufanya vibaya kwa wanafunzi kwenye somo la hesabu wanaohitimu kidato cha nne kunasababisha kudhohofisha fani hiyo kwa kukosekana kwa wahasibu wapya.

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno amesema matumizi ya tehama yanatajwa kuwa na umuhimu mkubwa kwa Wahasibu nchini ili kuendana na kasi ya utendaji kidigitali.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George B. Simbachawene akisoma hotuba ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2023 wa wahasibu na wakaguzi wa hesabu ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) uliofanyika katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia S. Temu akizungumza kuhusu mikakati iliyowekwa na Bodi ya NBAA ya kuwasimmamia Waasibu na Wakaguzi ili kuendana na Maadili ya Taaluma wakati wa mkutano mkuu wa mwaka 2023 ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) na kufanyika katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno akitolea ufafanuzi kuhusu Bodi hiyo inavyofanya kazi pamoja wakati wa mkutano mkuu wa wahasibu na wakaguzi wa Hesabu wa mwaka 2020 uliofanyika leo hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wa wahasibu na wakaguzi wa Hesabu wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George B. Simbachawene wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2023 wa wahasibu na wakaguzi wa hesabu uliofanyika katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George B. Simbachawene akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia S. Temu (kushoto) wakati wa ufunguzi wa wa mkutano mkuu wa mwaka 2023 wa wahasibu na wakaguzi wa hesabu uliofanyika katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George B. Simbachawene akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi, Menejimenti ya NBAA na baadhi ya Wadhamini wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2023 wa wahasibu na wakaguzi wa hesabu ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) uliofanyika katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...