Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa , Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Paul Makonda amempigia simu Waziri wa Maji Mhe. Juma Awesu na kumtaka kutolea ufafanuzi kero ya upatikanaji wa Maji safi na Salama katika Mji wa Katoro ulipo Kata ya Ludete Wilayani Geita mara baada ya kupokea changamoto hiyo kutoka kwa Wanachi hao aliozungunza nao njian akiwasili katika Mkoa wa Geita katika ziara yake ya Kikazi leo tarehe 11 Novemba, 2023.

Katika Majibu yake, Waziri Awesu amesema kuwa zilishatolewa fedha Tsh Bilioni 6.5 kwa mradi wa maji eneo hilo na mradi umeshavuka asilimi 90% na ndani ya wiki tatu mradi huo utakuwa umekamilika na Wakazi hao kunufaika kwa kupata maji safi na salama.

Aidha, Mhe. Awesu amesema Geita Mjini kuna fedha zaidi ya Tsh Bilioni 128 na Chato zaidi ya Tsh Bilioni 38 kwa miradi ya maji katika miji ambapo amesema katika jumla ya Vijiji 436 tayari Vijiji 333 huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama imefika.

Naye Mwenezi Makonda amempongeza Waziri Awesu kwa maelezo yake na kumtaka kuhakikisha anatekeleza ili kukamilisha ahadi yake aliyoitoa kwa Wananchi hao kwani kuwadanganya ni sawa na kuifanya CCM ionekane inajinadi katika uongo.

leo tarehe 11 Novemba, 2023 wakati aliposimama na kuzungumza na Wananchi wa Katoro katika Kata ya Ludete akiwa ziarani Mkoani Geita.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...