Watumishi Housing Investments(WHI) inashiriki maonesho ya WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA yanayofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha kuanza tarehe 20/11/2023 – 26/11/2023 ambapo watu mbalimbali wanajitokeza kupata elimu kuhusu uwekezaji na mambo mbalimbali yanayohusu fedha.Akizungamza katika banda la WHI Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Masoko WHI Bw. Raphael Mwabuponde amesema WHI inatumia nafasi hii kutoa elimu kuhusu huduma zitolewazo na Watumishi Housing Investments hasa elimu ya uwekezaji katika mfuko wa uwekezaji wa pamoja (FAIDA FUND) pamoja na mradi wao mpya unaotegemea kuanza hivi karibuni wa Mikocheni Apartments.


Bw. Raphael Mwabuponde amewaelezea watu mbalimbali kuhusu faida za mfuko wa Faida pamoja na jinsi ya kujiunga na huu mfuko kwa kupiga *152*00# then 1. Malipo na 6. WhI. Na kwa wale wanaotumia simu janja wanaweza jiunga kwa kutumia app ya “wekezawhi”


Vile vile Bw. Raphael Mwabuponde amesema kuwa tayari maombi ya kununua Apartment za mradi wa Mikocheni yameanza kupokelewa. Hivyo amesema kwa taarifa nyingi zaidi kuhusu huduma zitolewazo na WHI zinapatikana kwenye website “whi.go.tz” na kwenye account zao za social media .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...