Na mwandishi wetu Mwanza.

Wakazi wa Mwanza na watanzania kwa ujumla wameshauriwa kujiunga na bima ya afya inayotolewa na Airtel Money kwa kushirikiana na Kampuni za Jubilee Health Insurance na Axieva kwani gharama zake ni nafuu na kujiunga kwake ni rahisi.

Meneja Huduma wa Airel Money, Bi. Hellen Lyimo aliyasema hayo jijini Mwanza jana, wakati wa kampeni yenye lengo la kuhamasisha watanzania kujiunga na huduma hiyo iliyopewa jina la ‘Afya Bima’ ili kuokoa maisha yao na wategemezi wao pindi wauguapo na pia kupunguza mzigo wa gharama za matitabu.

“Watu wengi wanashindwa kujiunga na bima za afya kutokana na mifumo mingi ya bima hizi kutaka wanaohitaji kujiunga kufika katika vituo vya watoa huduma, uende na makaratasi ya utambulisho, kujaza fomu na taratibu nyingine ambazo zinaonekana kuwasumbua wanaohitaji kujiunga na huduma za bima ya afya.

“Kwa kupitia Afya Bima ya Airtel Money, Jubilee Health Insurance na Axieva, mteja ama mtanzania hata akiwa nyumbani ama safarini, akiwa na familia yake anachohitaji ni kuwa na simu ya aina yoyote ya mkononi na kisha kufanya maamuzi ya kununua aina yoyote ya kifurushi cha bima ya afya akitakacho kulingana na mahitaji yake”, alisema Bi. Hellen.

Akizunguza wakati wa kampeni hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogowadogo na Biashara Matawini wa Kampuni ya Jubilee Health Insurance, Bwana Wilbert Mwairo alisema uamuzi wa kuungana na Airtel Money pamoja na Axieva kuanzisha huduma ya Afya Bima, unaunga mkono juhudi za serikali sambamba na muswada wa Bima ya Afya kwa Wote uliosainiwa hivi karibuni na Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

“Tuliona sisi kama Jubilee Health Insurance hatuna uwezo wa kuwafikia watanzania zaidi wa milioni 65 kwa haraka hivyo kwa kushirikiana na Airtel yenye wateja zaidi ya milioni 17, tuna imani huduma hii yenye gharama nafuu zaidi kiasi cha shs 300 kwa mwezi ama 3500 kwa mwaka itawasaidia watanzania wengi wenye kipato cha chini kujiunga hivyo kuongeza idadi ya watanzania wenye bima za afya na pia kuwa katika mfumo unaowathibitishia uhakika wa kupata matibabu wao na familia zao.

“Hata hivyo, kwenye vitu ambavyo serikali inaweza kuboresha na kufanya upatikanaji wa bima za afya kuwa wenye tija ni kusimamia gharama za utoaji wa huduma za afya mahospitalini kwani hospitali nyingi zina gharama kubwa hivyo kusababisha bima za afya kuuzwa kwa bei kubwa pia, gharama za matibabu zikiwa chini zitashusha pia gharama za bima za afya”, alisema Bwana Mwairo.

Wakizungumza mahali wapo baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza, Daudi Joseph na Mussa Rajabu walishukuru ujio wa Afya Bima ya Airtel Money, Jubilee Health Insurance na Axieva wakisema baadhi ya masharti ya kujiunga na baadhi ya bima za afya kutoka katika baadhi ya makampuni hayaakisi hali ya kipato cha watanzania wengi wenye vipato vya chini hususan wanaoishi maeneo ya vijijini.

Huduma ya Afya Bima imekuja na bima za afya za aina tatu ambazo ni Afya Poa, Afya Supa na Afya Dhahabu ambazo zote zinapatikana kwa kupitia huduma ya Airtel Money. 

Meneja Huduma wa Airtel Money, Bi. Helen Lyimo (kulia) akitoa maelezo kwa mkazi Ilemela, Mwanza, Bwana Masagida Ndutu, jinsi ya kujiunga na huduma ya Afya Bima kupitia simu yake ya kiganjani, katika hafla ya kutambulisha huduma hiyo kwa wakazi mkoa huo iliyofanyika katika viwanja vya kituo cha mabasi Buzuruga, jana. Huduma ya Afya Bima inapatikana kwa ushirikiano wa Airtel Money, Jubilee Health Insurance na Axieva.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogowadogo na Biashara Matawini wa Kampuni ya Jubilee Health Insurance, Bwana Wilbert Mwairo, akitoa maelezo kuhusu faida za huduma ya Afya Bima inayotolea kwa ushirikiano katika ya Airtel Money, Axieva na kampuni yao katika hafla yenye lengo la kuhamasisha watanzania kujiunga na bima, mjini Mwanza jana. 

Baadhi ya wawakilishi wa Kampuni za Airtel, Jubilee Health Insurance na Axieva, wakitambulisha rasmi huduma ya Afya Bima kwa wakazi wa Mkoa wa Mwanzaa, katika hafla iliyofanyika katika kituo cha mabasi cha Buzuruga, mkoani humo jana.
Meneja Huduma kutoka Airtel, Helen Lyimo (kulia) akitoa maelezo kwa mkazi wa Mwanza, Bi. Mariam Mashauri, jinsi ya kujiunga na huduma ya Afya Bima kupitia simu yake ya kiganjani, katika hafla ya kutambulisha huduma hiyo kwa wakazi wa mkoa huo iliyofanyika katika viwanja vya kituo cha mabasi Buzuruga, jana. Huduma ya Afya Bima inapatikana kwa ushirikiano wa Airtel Money, Jubilee Health Insurance na Axieva.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...