Dar Es Salaam, Disemba 6, 2023: Kampuni ya bima ya Jubilee imeshirikiana na Axieva pamoja na Airtel Money kuzindua BIMA AFYA ambayo ni Bima ya afya nafuu kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma za Bima ya mtu mmoja au kwa familia.


Ushirikiano wa Airtel Money, na kampuni za Bima Jubilee na Axieva unalenga kuleta Mapinduzi makubwa kwenye sekta ya bima ya afya kwa kutoa huduma ambazo ni nafuu, zenye kukidhi mahitaji ya soko ni rahisi kupatikana kwa kutumia huduma ya Airtel Money. Kulingana na utafiti wa Finscope Tanzania ya mwaka 2023, ni Watanzania 3.5 milioni wenye bima ya afya kulinganisha na Watanzania milioni 4.2 kwa mwaka wa 2017.

Asilinia 75 ya Watanzania ambao wanamiliki simu za mkononi wataweza kufaidika na huduma hii ambayo imetengenezwa vizuri kwa matuzi ya bima ya afya kwa njia ya simu za mkononi. Suluhisho hili AFYA BIMA litawanufaisha mamilioni ya Watanzania ambao wamekosa huduma ya bima ya afya kutokana na changamoto mbali mbali kama vile upatikanaji wake au urahisi wa upatikanaji wa bima ya afya.

Kwa kupitia menu ya Airtel Money *150*60#, wateja wa Artel wataweza kupata huduma za AFYA BIMA kwa urahisi na unafuu kama ifuatavyo:

Kutakuwa na mpango wa Afya Poa ambayo ni pesa taslimu zinazolipwa kwa mteja ambaye atakuwa amelazwa, fidia hii italipwa kwa kiasi cha kuanzia Tzs 20,000 mpaka Tzs 50,000 na hii itahesabiwa kuanzia siku ya pili pale mteja wa bima ya Afya Poa atakapokuwa amelazwa. Mteja ataweza kufaidika na bima hii pale atapokuwa amekata bima kwa kiasi cha Tzs 300 na Tzs 3,000 kwa mwezi.

Afya Supa itawapa wateja waliolazwa huduma ya bila malipo pindi wanapolazwa gharama ya matibabu ya hadi kiasi Tzs 5,000,0000 na Tzs 2,000,000 kwa akina mama wanaojifungua kwa mwaka na hii inaweza kumjulisha mwenza na watoto mpaka wategemezi watano hii mteja ataipata kwa kulipia TZS 15,000 akiwa mwenyewe. Atalipa TZS 30,000 kwa mwezi ikiwa anafamilia wa wategemezi wanne, au mteja atalipia TZS 45,000 ikiwa anawategemezi 7 kwa mwezi.

Faida ya mwisho ni Afya Dhahabu ambayo itatoa huduma ya bila malipo kwa wagonjwa ambao waliolazwa watapata matitabu ya gharama hadi Tzs 8,000,000 na wagonjwa wa kutwa watapata gharama ya matibabu ya hadi Tzs 600,000 na akina mama wanaojifungua watalipiwa gharama za hadi Tzs 2,000,000 kwa mwaka ambapo bima hii kwa mwezi ni Tzs 30,000.

Suluhisho la bima hizi imetengenezwa kuwa jumuishi ikilenga watu wa rika zote kwa umri wa chini wa miaka 18 na wa juu zaidi miaka 65.

Afya Supa na Afya Dhahabu zina manufaa kwa wateja kwani wanapata matibabu bila gharama yeyote. Wateja wetu watakuwa wanaingia tu hospitalini na kupata huduma ya matibabu bila kulipia na kufurahi huduma ya Afya Bima kwa kwa bima waliochagua au kulipia.

Kwa upande wa Afya Poa inalenga kufidia kiasi ambacho mteja anakuwa amekosa kukipata kutoka kwenye kazi zake pale anapokuwa amelazwa. Gharama hizi mteja anarudishiwa bila shida yeyote kwa kupiga menu ya Airtel Money *150*60# kisha bonyesa 6 kufuata maelekezo.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huu, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bima ya Jubilee Dkt Harold Adamson alisema “Tunayo furaha kuingia kwenye ushirikiano huu kati yetu ya wenzetu Airtel Money pamoja na Axieva ambayo utaleta Mapinduzi makubwa kwenye sekta ya bima hapa nchini. Tunaamini ya kwamba huduma hii ya bima ya afya imekuwa wakati muafaka na lengo lake pia ni kuunga mkono juhudi za serikali za kuifanya bima ya afya kupatikana kwa kila Mtanzania na hivyo kuwa suluhisho kubwa na muhimu kwenye sekta ya afya.

“Tunaleta huduma hizi kubadilisha na kuboresha sekta ya bima ya afya. Tuna bidhaa bunifu kama Afya Poa, Afya Supa na Afya Dhahabu ambazo kila moja ina faida zake ambazo zinalenga kunufaisha mteja pamoja na Watanzania kwa ujumla” alisema Dkt Adamson

‘Kwa ushirikiano huu wa kwetu na Airtel Tanzania pamoja na Axieva Afrika, sio tu kwamba tunafanikisha huduma za matibabu kwa Watanzania lakini pia tufanya mtiririko mzima kuwa rahisi kwa kutumia teknolojia’, aliongeza Dkt Adamson huku akisema kuwa wateja wa Airtel wataweza kupiga *150*60# na kupata huduma hizi za bima.

Mkurugenzi Mtendaji wa Axieva Afrika Lab Gaurav Dhingra alisema ‘Lengo letu ni kutengeneza mfumo endelevu ambao unaweza kukidhi vyema na kuwezesha jamii kwa kutumia teknolojia. Ushirikiano huu ni mfano mmoja wa jinsi mtiririko mzima unaweza kubadilisha kwa kutumia digitali ili kurahishisha, ufikiaji, utoaji na ufanisi wa bima ya afya kwa mamilioni ya wateja wetu.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema “Kwa mara nyingine tunayo furaha kuleta ubunifu wa kipekee kwenye mfumo wa kidigitali wa bima ya afya hapa Tanzania kupitia Ubia wetu na kampuni hizi za bima. Ushirikiano huu na Axieva pamoja kampuni ya bima ya Jubilee unafanya bima ya afya kuwa ya kidigitali, ni hatua kubwa kwenye maendeleo yetu na ya nchi.

Huduma ya bima ya afya, mpaka leo imekuwa ni moja ya huduma ambazo zimekuwa hazitumiki ipasavyo kutoka na mlolongo wa upatakanaji wake, unafuu na ulipaji tunaoleta leo kupitia AFYA BIMA kwa kutumia huduma yetu ya Airtel Money itaondoa changamoto zote hizo na kwa sasa mteja ataweza kupata huduma ya bima ya afya kwa kubonyeza tu simu yake akiwa popote.

“Lengo letu ni kuwafanya wateja wa Airtel na Watanzania kwa ujumla kuwa na bima ya afya na kuishi maisha ambayo hayana wasi wasi” ‘aliongeza Singano.



Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma ya AFYA BIMA ambao ni ushirikiano baina ya Airtel Money, Kampuni ya Bima ya Jubilee na Axieva. Ushirikiano huu unalenga kurahihisha upatikanaji wa bima ya afya nchini kwa mtu mmoja au kwa familia.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano akihutubia waandishi wa Habari pamoja na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa huduma ya AFYA BIMA ambao ni ushirikiano baina ya Airtel Money, Kampuni ya Bima ya Jubilee na Axieva. Ushirikiano huu unalenga kurahihisha upatikanaji wa bima ya afya nchini kwa mtu mmoja au kwa familia. Walioketi ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bima ya Jubilee Dkt Harold Adamson (kushoto), Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania (TIRA) Kanda ya Mashariki Bahati Ogolla na Mkurugenzi Mtendaji wa Axieva Afrika Lab Gaurav Dhingra (kulia).



Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania (TIRA) Kanda ya Mashariki Bahati Ogolla (wa pili kulia) akizunguzwa gurudumu kuashiria kuzindua huduma ya AFYA BIMA ambayo ni ushirikiano baina ya Airtel Money, kampuni ya Bima ya Jubilee na Axieva ushirikiano ambao unalenga la kurahisisha upatikanaji wa huduma za Bima ya mtu mmoja au kwa familia. Ushirikiano huu pia unalenga asilinia 75 ya Watanzania ambao wanamiliki simu za mkononi kuweza kufaidika na huduma hii ambayo imetengenezwa vizuri kwa matumizi ya bima ya afya kwa njia ya simu za mkononi. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Axieva Afrika Lab Gaurav Dhingra, wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano na kulia Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bima ya Jubilee Dkt Harold Adamson.

Mkurugenzi Mtendaji wa Axieva Afrika Lab Gaurav Dhingra akihutubia waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi huduma ya AFYA BIMA ambao ni ushirikiano baina ya Airtel Money, Kampuni ya Bima ya Jubilee na Axieva. Ushirikiano huu unalenga kurahihisha upatikanaji wa bima ya afya nchini kwa mtu mmoja au kwa familia.Walioketi ni Mkurugenzi Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bima ya Jubilee Dkt Harold Adamson (kushoto).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...