WAKAZI watatu wa Kigamboni jijinii Dar es salaam wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa kilogramu 882.71 na Methamphetamine zenye uzito wa kilogramu 2167.29.

Washitakiwa hao ni mfanyabiasha Najim Mohamed (52) , mfanyabiasha Maryam Mohamed (50) na Juma Abbas (37) ambaye ni msaidizi wa kazi za ndani.

Akisoma Mashtaka yao leo tarehe 29 Disemba, 2023 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Aaron Lyamuya, wakili wa serikali mwandamizi Hemed Halfan
ameniambia Mahakama kuwa, katika shtaka la kwanza inadaiwa kuwa, Disemba 15, 2023 washtakiwa wote wakiwa katika eneo la Kibugumo shule walikutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa kilogramu 882.71.

Katika shtaka la pili alidai kuwa katika eneo hilo na siku hiyo washtakiwa hao walikutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya Methamphetamine zenye uzito wa kilogramu 2,167. 29.

Baada ya washtakiwa hao kusomewa mashtaka yanayowakabili, hakimu Lyamuya alisema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hivyo washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote hadi watakapoitwa Mahakama Kuu.

Hata hivyo, wakili Halfan amesema upelelezi wa kesi bado haujakamilika na kuiomba Mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili kutajwa.

Kesi hiyo imehairishwa hadi Januari 11, 2024 kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa wote watatu wamerudishwa rumande kwani kesi inayowakabili haina dhamana.

Washtakiwa hawa watatu ni kati ya watuhumiwa saba waliotangazwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika tarehe 27 Disemba 2023, kuhusika na jumla ya kilo 3,182 za dawa za heroin na methamphetamine.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...