NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amemuagiza Meneja wa RUWASA wa Wilaya ya Masasi aweze kuhakikisha vijiji nane vya Mnavira, Manyuri, Mkaliwata Chipingo, chikolopola, Mapili, Namyomyo na Raha Leo vinapata huduma ya maji kadri ya usanifu wake.
Mhandisi Mahundi ameyasema hayo Disemba 16, 2023 Mkoani Mtwara wakati wa ziara yake ambayo ametembelea na kukagua utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa maji wa Chipingo-Mkaliwata wenye thamani ya shilingi Bilioni 3.9
Kadhalika Mhandisi Mahundi ameagiza vijiji hivyo viweze kufikiwa na huduma ya maji kabla ya mwezi Februari, 2024.
Naye Mbunge wa Jimbo la Lulindi Mheshimiwa Issa Mchungaela ameishukru Serikali kwa kutekeleza mradi huo, kupitia chanzo cha maji cha Mto Ruvuma
Hata hivyo Mradi wa maji wa Chipingo-Mkaliwata ni miongoni mwa miradi ambayo inatumia chanzo cha maji cha Mto Ruvuma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...