Na John Walter-Hanang'

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack ametembelea Kijiji cha Gendabi eneo lililoathirika na mafuriko, maporokoko ya tope na magogo Wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara na kukabidhi misaada mbalimbali kwa waathiriwa iliyotolewa na wadau mbalimbali mkoani humo.

Amesema wametoka Lindi kwa ajili ya kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan na mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga na wana Hanang' kwa ujumla katika wakati mgumu wanaoupitia kwa sasa.

Akitoa salamu za pole RC Telack amewakumbusha wananchi waendelee kumuomba Mungu mvua zinazonyesha ziwe za kiasi na za baraka.

Telack amemkabidhi Misaada hiyo mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga vikiwemo vijora 300 kwa ajili ya wanawake, kanga doti 200, mafuta ya kupaka katoni 30, taulo za kike katoni 14, Pempasi za watoto pisi 840, nguo za ndani za wanawake na wanaume pamoja na za watoto wa kike na wa kiume pisi 324,unga wa lishe kwa ajili ya watoto wadogo kilo 48 na maziwa ya laktojeni one kopo 12 kwa ajili ya watoto wenye umri chini ya miezi sita.

Aidha, amempongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kutoa huduma zote za kijamii kwa haraka kwa waathiriwa katika maafa wilayani Hanang' ikiwemo maziko na matibabu bure.

Mara baada ya kupokea misaada hiyo, Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amempongeza na kumshukuru mkuu wa mkoa wa Lindi Zainab Telack kwa namna ambavyo wameguswa na janga hilo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha misaada yote iliyotolewa inawafikia waathirika wote.

Vilevile Mhe. Sendiga amempongeza Telack kwa unyenyekevu wake wa kufika na kuwafariji wananchi wa Kijiji cha Gendabi, akisema ni mfano bora na wa kuigwa na wengine.

Aidha walitembelea maeneo yaliyoathirika na kuona miundombinu iliyoharibiwa, na nyumba za watu zilivyosombwa na maporomoko hayo.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amewaomba Watanzania wenye mapenzi mema kuendelea kutoa misaada yao kwa ajili ya kuwafariji walioathiriwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...