Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP. Theopista Mallya Desemba 03, 2023 ameongoza Harambee ya kuchangisha pesa kwa lengo la kukamilisha ujenzi wa nyumba ya Mapadre Parokia ya Mtakatifu Hellena Jimbo kuu la Mbeya kwa Paroko Isaya Nyambo lililopo Igamba Wilayani Mbozi.

Kamanda Mallya akiwa kama mgeni rasmi katika harambee hiyo aliwezesha kuchangisha kiasi cha shilingi Milioni 3 na Laki Tano kwaajili ya kununua mbao za kupaulia jengo hilo ili kukamilisha ujenzi wa nyumba hiyo.

Sambamba na harambee hiyo Kamanda Mallya alipata nafasi ya kuzungumza na waamini wa Kanisa hilo na kuwataka waamini hao na jamii nzima kukemea vitendo vya RUSHWA pamoja na kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia, pia kukemea vitendo vilivyo kinyume na Mila na Desturi za Taifa letu,hasa vinavyosababisha ukatili dhidi ya watoto.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...