Pamela Mollel, Arusha .

Halmashauri ya Jiji la Arusha imepokea msaada wa viti maalumu kwa walemavu vipatavyo 10 ( Viti vya Mwendo kasi ) kutoka katika Taasisi ya Kijamii ya Conservation Foundation Tanzania ( CFT ) Vyenye thamani ya Shilingi milioni tano na nusu za kitanzania.

Akipokea msaada huo Juma Hamsini Mkurugenzi wa jiji la Arusha amesema waliomba msaada huo wakati wa mbio za mwenge wa uhuru Jijini Arusha kutoka kwa mdau huyo kutokana na uhitaji uliyokuwepo wa viti vya mwendonkasi kwa baadhi ya watumishi wa Halmashauri hiyo, kwenye Zahati na Hosptali za Jiji hilo pamoja na baadhi ya familia zinazo ficha watoto walemavu na kisha kuanza kuomba msaada.

Hamsini ameeleza kuwa mbali na maombi mengi ya watanzania wenye watoto walemavu pia kuna ulemavu wa ukubwani ambao unaweza kumpata mtu yeyote pia na wale wagonjwa wa kisukari ambao imefikia hatua ya kushindwa kutembea na mahitaji hayo yote yanakusanywa na maendeleo ya Jamii na wao kama halmashauri wanaangalia sehemu zenye umuhimu zaidi

Aidha Mkurugenzi Hamsini aliweka bayana mikakati kabambe ya kuounguza changamoyo hiyo katika Jiji la Arusha kuwa wamelidhia kwa pamoja na baraza la Madiwani kuanzia mwaka wa fedha 2024 / 25 kutenga fedha za miradi ya maendeleo kiasi cha Shilingi Milioni 20 kwa ajili yakusaidia watu wenye ulemavu

Kwa upande wake Bi, Rose Bekker, ambaye amemwakilisha Mkurugenzi wa Conservation Foundation Tanzania Mrs. Jan Ramoni, amesema taasisi yake imetoa jumla ya viti 10 vyenye thamani ya zaidi ya milioni 5 ambapo kwa kiti kimoja kina gharimu kiasi cha shilingi laki tano na nusu za kitanzani.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...